Mafundisho na Maagano 2021
Machi 8–14. Mafundisho na Maagano 23–26: “Imarisha Kanisa”


“Machi 8–14. Mafundisho na Maagano 23–26: ‘Imarisha Kanisa,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)

“Machi 8–14. Mafundisho na Maagano 23–26,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2021

Picha
Emma Smith

Machi 8–14

Mafundisho na Maagano 23–26

“Imarisha Kanisa”

Unaposoma Mafundisho na Maagano 23–26, andika misukumo unayopokea kutoka kwa Roho Mtakatifu. Ni kwa jinsi gani unaweza kutumia ushauri katika ufunuo huu kuimarisha ufuasi wako binafsi na pia Kanisa?

Andika Misukumo Yako

Baada ya Kanisa kuundwa, Watakatifu walikabiliana na changamoto mpya—kueneza injili na kuwaimarisha wale ambao walikuwa wamekwishajiunga na Kanisa, yote wakati mateso yakiendelea kuongezeka. Emma Smith alishuhudia upinzani moja kwa moja. Katika mwezi wa Juni 1830, Emma na wanafamilia ya Knight walitamani kubatizwa. Lakini maadui wa Kanisa walijaribu kuvuruga kile ambacho kingekuwa uzoefu mtakatifu. Kwanza waliharibu bwawa ambalo lilikuwa limejengwa kutoa maji yenye kina cha kutosha kwa ajili ya ubatizo. Hata baada ya bwawa kukarabatiwa, watesi walikusanyika kutoa vitisho na kuwafanyia mzaha wale waliokuwa wanabatizwa. Kisha, wakati Joseph alipokuwa karibu kuwathibitisha waumini wapya, alishikwa kwa kusababisha vurugu katika jamii kwa kuhubiri kuhusu Kitabu cha Mormoni. Ilionekana kama mwanzo usio na matumaini kwa Kanisa jipya lililorejeshwa la Bwana. Lakini katikati ya mashaka na mageuzi haya, Bwana alitoa maneno ya thamani ya ushauri na kutia moyo, ambayo yanawakilisha “sauti Yake kwa wote” (Mafundisho na Maagano 25:16).

Ona pia Saints, 1:89–90, 94–97.

Picha
ikoni ya kujifunza binafsi

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Binafsi Maandiko

Mafundisho na Maagano 23–26

Ninaweza kusaidia kuliimarisha Kanisa la Bwana.

Leo, takribani miaka 200 baada ya Kanisa la urejesho kuanzishwa, haja ya “kuliimarisha Kanisa” inaendelea (Mafundisho na Maagano 23:3–5). Na kazi hii sio tu kwa ajili ya Joseph Smith, Oliver Cowdery, au viongozi wetu wa Kanisa wa sasa—ni kwa ajili yetu sote. Kote katika kujifunza kwako Mafundisho na Maagano 23–26, tafakari ushauri Bwana aliowapa waumini wa Kanisa wa mwanzo ili kuwasaidia kuliimarisha Kanisa. Unahisi ni nini Bwana anakutaka wewe kufanya ili kushiriki katika juhudi hii?

Mafundisho na Maagano 24

Mwokozi anaweza kuniinua “juu ya mateso [yangu].”

Kuongoza Kanisa wakati wa kipindi cha mateso makali lazima ilikuwa mzigo mzito kwa Joseph Smith. Tafuta maneno ya Bwana ya kutia moyo kwake katika Mafundisho na Maagano 24.

Maandiko yafuatayo yanapendekeza nini kwako kuhusu jinsi Mwokozi anavyoweza kukuinua kutoka kwenye mateso yako?

Mafundisho na Maagano 24:1–3 

Mafundisho na Maagano 24:8 

Mafundisho na Maagano 121:7–8 

Isaya 40:28–31 

Mosia 24:14–15 

Ni kwa jinsi gani Yesu Kristo alikuinua kutoka kwenye mateso yako? Unaweza kufanya nini kuendelea kutafuta msaada Wake wakati wa kipindi cha matatizo?

Picha
Yesu Kristo akiwaponya watu

Aliponya Magonjwa Mengi ya Kila Aina, na J. Kirk Richards

Mafundisho na Maagano 25

Emma Smith ni “mwanamke mteule.”

Wakati Emma Hale alipoolewa na Joseph Smith, kwa vyovyote alijua angekuwa akifanya dhabihu. Alikuwa anaenda kinyume na matamanio ya baba yake na kupoteza maisha ya raha kwa ajili ya maisha ya kutokuwa na uhakika. Anaweza kuwa alijiuliza nini Bwana alitegemea kutoka kwake katika kazi ya Urejesho. Tafuta majibu Bwana aliyoyatoa katika Mafundisho na Maagano 25. Tazama maneno ya Bwana katika mstari wa 16—je, unapata chochote katika sehemu hii ambacho unahisi ni “sauti Yake kwako [wewe]”?

Ona pia “An Elect Lady” (video, ChurchofJesusChrist.org); “Wewe ni Mwanamke Mteule,” Ufunuo katika Muktadha, 33–39; Joy D. Jones, “Mwito Hasa wa Kiungwana,” Ensign au Liahona, Mei 2020, 15–18.

Mafundisho na Maagano 26:2

Kauli ya pamoja ni nini?

Wakati waumini wanapopokea wito au kutawazwa kwenye ukuhani katika Kanisa, tunakuwa na fursa rasmi ya kuwakubali kwa kuinua mikono yetu kama ishara ya kuwaunga mkono. Kanuni ya kuonesha uungaji mkono na ukubali wa watu inaitwa kauli ya pamoja. Kama Rais Gordon B. Hinckley alivyofundisha, “Utaratibu wa kuidhinisha ni zaidi ya kawaida ya dini ya kuinua mkono. Ni dhamira ya kuthibitisha, kuunga mkono, kusaidia wale ambao wamechaguliwa” (“This Work Is Concerned with People,” Ensign, Mei 1995, 51).

Picha
ikoni ya kujifunza kama familia

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko kama Familia na Jioni ya Nyumbani

Mafundisho na Maagano 23:6.Kwa nini Bwana anatutaka sisi tusali “katika familia [zetu], na miongoni mwa rafiki [zetu], na katika sehemu zote”? Ni nini wimbo “Love Is Spoken Here” (Kitabu cha nyimbo za Watoto,190)—au wimbo mwingine kuhusu sala—unatufundisha kuhusu nguvu ya sala?

Ona pia 2 Nefi 32:8–9,; 3 Nefi 18:18–23.

Mafundisho na Maagano 24:8.Je, ingeweza kusaidia kwa familia yako kuzungumza kuhusu inamaanisha nini kuwa “mvumilivu katika mateso”? Kama una watoto wadogo, inaweza kuwa jambo la kufurahisha kutengeneza tena jaribio ambalo Rais Dieter F. Uchtdorf alielezea katika “Endelea katika Uvumilivu” (Ensign au Liahona, Mei 2010, 56; ona pia video kwenye ChurchofJesusChrist.org). Ni nini Mafundisho na Maagano 24:8 inatufundisha kuhusu uvumilivu? Ni kwa jinsi gani Bwana anatusaidia kuwa wavumilivu katika mateso yetu?

Mafundisho na Maagano 25:11–12.Pengine mngeimba wimbo unaopendwa na kila mwanafamilia na kuzungumza kuhusu kwa nini ni “wimbo wake wa moyoni.” Je, ni kwa jinsi gani nyimbo hizi ni sawa na “sala kwa [Mungu]”?

Mafundisho na Maagano 26:2.Inaweza kuwa ya kusaidia kutazama “Kauli ya Pamoja” katika Mwongozo kwenye Maandiko (scriptures.ChurchofJesusChrist.org). Ni kwa jinsi gani tunaonesha msaada wetu kwa viongozi wetu?

Kwa mawazo zaidi kwa ajili ya kuwafundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Msingi.

Wimbo uliopendekezwa: “Lift Up Your Voice and Sing,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 252 (ona “Mawazo ya Kuboresha Kujifunza Maandiko kwa Familia Yako”).

Picha
ikoni ya sauti za urejesho

Sauti za Urejesho

Emma Hale Smith

Maneno ya Bwana kwa Emma Smith yaliyorekodiwa katika Mafundisho na Maagano 25 yanafunua jinsi Bwana alivyohisi kuhusu yeye na michango ambayo angeweza kufanya kwenye kazi Yake. Lakini Emma alikuwa mtu wa namna gani? Tunajua nini kuhusu tabia yake, mahusiano yake, nguvu zake? Njia moja ya kuweza kumjua “mwanamke huyu mteule” (Mafundisho na Maagano 25:3) ni kusoma maneno ya watu ambao walimjua kibinafsi.

Picha
Emma Smith

Emma Smith, na Lee Green Richards

Joseph Smith Mdogo, mumewe Emma

Picha
Joseph Smith

“Pamoja na furaha isiyoelezeka, na ni safari ya furaha iliyoje iliyojaa kifuani mwangu, wakati nilipomchukua kwa mkono wangu, usiku ule, mpendwa wangu Emma—ambaye alikuwa mke wangu, hata mke wa ujana wangu; na chaguo la moyo wangu. Nyingi zilikuwa ngurumo za akili zangu wakati nilipotafakari kwa muda matukio mengi tuliyoitwa kuyapitia. Uchovu, na kazi za taabu, huzuni, na mateso, na furaha na faraja ya mara kwa mara vilitawanyika katika njia zetu na vikapendezesha jukwaa letu. Ee! ni hisia iliyoje ya mchanganyiko wa mawazo ikijaa akilini mwangu kwa muda, Tena yuko hapa, hata katika matatizo makubwa, bila kukata tamaa, imara, na bila kutetereka, asiyebadilika, Emma mwenye moyo wa kupenda.”1

Lucy Mack Smith, mama mkwe wake Emma

Picha
Lucy Mack Smith

“Emma wakati huo alikuwa kijana, na, kwa asili mwenye ari, moyo wake wote ulikuwa katika kazi ya Bwana, na alihisi kutokupenda kingine chochote isipokuwa kanisa na lengo la ukweli. Chochote mikono yake ilichopata kufanya, alifanya kwa uwezo wake na hakuuliza maswali ya kichoyo ‘Je, nitanufaika zaidi kuliko yeyote yule?’ Kama wazee wangepelekwa mbali kuhubiri, alikuwa wa kwanza kujitolea huduma zake kusaidia katika kuwapa mavazi kwa ajili ya safari zao, kuacha ufukara wake mwenyewe uwe kile wanachoweza kuwa.”2

“Sijawahi kuona mwanamke katika maisha yangu, ambaye angevumilia kila aina ya uchovu na shida, kutoka mwezi hadi mwezi, na kutoka mwaka hadi mwaka, kwa ule ujasiri usio na woga, ari na subira, ambavyo amefanya siku zote; kwani ninajua kile ambacho alipaswa kuvumilia; kwamba alikuwa ametupwa katika bahari ya kutokuwa na uhakika; kwamba amekabiliana na dhoruba ya mateso, na amepambana na ghadhabu za binadamu na ibilisi, mpaka amemezwa kwenye bahari ya matatizo ambayo [ingeweza] kumpeleka chini takribani mwanamke mwingine yeyote.”3

Joseph Smith Mkubwa, baba mkwe wake Emma

Baraka za Patriaki za Emma, zilizotamkwa na Joseph Smith Mkubwa, ambaye alikuwa anahudumu kama patriaki wa Kanisa:

“Emma, mkwe wangu, umebarikiwa na Bwana, kwa ajili ya uaminifu wako na ukweli: utabarikiwa pamoja na mumeo, na kufurahi katika utukufu ambao utakuja juu yake: Nafsi yako imeteseka kwa sababu ya uovu wa binadamu katika kutafuta uharibifu wa mwenza wako, na nafsi yako yote imetolewa katika sala kwa ajili ya wokovu wake: shangilia, kwani Bwana Mungu wako amesikia maombi yako.

“Umesikitishwa kwa ugumu wa mioyo ya nyumba ya baba yako, na umetamani wokovu wao. Bwana ataheshimu kilio chako, na kwa hukumu zake atasababisha baadhi yao kuona upumbavu wao na kutubu dhambi zao; lakini itakuwa kwa mateso kwamba wataokolewa. Utaishi siku nyingi; ndio, Bwana atakutunza mpaka utakapotosheka, kwani utamwona Mkombozi wako. Moyo wako utashangilia katika kazi kubwa ya Bwana, na hakuna yeyote atakayeitoa shangwe yako.

“Utakumbuka siku zote rehema kuu za Mungu wako katika kukuruhusu wewe kuandamana na mwanangu wakati malaika alipotoa kumbukumbu ya Wanefi kwenye uangalizi wake. Umeona huzuni nyingi kwa sababu Bwana amewachukua watoto wako watatu: katika hili wewe hutalaumiwa, kwani anajua tamaa zako safi za kulea familia, kwamba jina la mwanangu liweze kubarikiwa. Na sasa, tazama, Ninakuambia, kwamba hivi ndivyo asemavyo Bwana, kama utaamini, bado utabarikiwa katika jambo hili na utapata watoto wengine, kwa ajili ya shangwe na kuridhika kwa nafsi yako, na kwa shangwe ya rafiki zako.

“Utabarikiwa kwa ufahamu, na kuwa na nguvu ya kuelekeza jinsia yako. Fundisha familia yako uadilifu, na njia njema ya maisha kwa watoto wako, na malaika watakatifu watakulinda: na utaokolewa katika ufalme wa Mungu; hivyo ndivyo. Amina.”4

Picha
Emma Smith na watoto wake

Emma Smith na watoto wake. Wakati wa Kucheka, na Liz Lemon Swindle

Picha
Emma Smith akiandika

Nyimbo za Kanisa za Emma, na Liz Lemon Swindle

Chapisha