Mafundisho na Maagano 2021
Machi 15–21. Mafundisho na Maagano 27–28: “Mambo Yote Lazima Yafanyike katika Utaratibu”


“Machi 15–21. Mafundisho na Maagano 27–28: ‘Mambo Yote Lazima Yafanyike katika Utaratibu,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)

“Machi 15–21. Mafundisho na Maagano 27–28,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2021

Joseph Smith

Machi 15–21

Mafundisho na Maagano 27–28

“Mambo Yote Lazima Yafanyike katika Utaratibu”

Mzee D. Todd Christofferson alisema kwamba unapojifunza maandiko na kuandika misukumo, “utakuwa unatoa sehemu katika moyo wako kwa ajili ya neno la Mungu, na atazungumza na wewe” (“Nawe Utakapoongoka,” Ensign au Liahona, Mei 2004, 11).

Andika Misukumo Yako

Ufunuo ulikuwa bado kwa kiasi wazo jipya kwa Watakatifu wakati Urejesho ukiendelea kujifunua. Waumini wa mwanzo wa Kanisa walijua kwamba Nabii Joseph Smith angeweza kupokea ufunuo kwa ajili ya Kanisa, lakini wengine pia wangeweza? Maswali kama haya yakawa ya ukosoaji wakati Hiram Page, mmoja wa Mashahidi Wanane wa mabamba ya dhahabu, alipoamini alikuwa amepokea funuo kwa ajili ya Kanisa. Watakatifu wengi waaminifu waliamini kwamba funuo hizi zilikuwa kutoka kwa Mungu. Bwana alijibu kwa kufundisha kwamba katika Kanisa Lake “Mambo yote lazima yafanyike katika utaratibu” (Mafundisho na Maagano 28:13), ambayo ilimaanisha kuwa na mmoja tu “aliyeteuliwa kupokea amri na mafunuo” kwa ajili ya Kanisa lote (Mafundisho na Maagano 28:2). Hata hivyo, wengine wangeweza kupokea ufunuo binafsi kwa ajili ya sehemu zao katika kazi ya Bwana. Kwa kweli, maneno ya Bwana kwa Oliver Cowdery ni ukumbusho kwetu sote: Na “itatolewa kwako … juu ya nini utakachofanya” (Mafundisho na Maagano 28:15).

Ona pia “Mambo Yote Lazima Yafanyike Katika Utaratibu”,” Funuo katika Muktadha, 50–53.

ikoni ya kujifunza kibinafsi

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko Kibinafsi

Mafundisho na Maagano 27:1–4

Ninapaswa kushiriki sakramenti jicho likiwa kwenye utukufu wa Mungu.

Sally Knight na Emma Smith walibatizwa Juni 1830, lakini kuthibitishwa kwao kulivurugwa na kundi la majambazi. Miezi miwili baadae, Sally na mumewe, Newel, walikuja kumtembelea Emma na Joseph, na iliamuliwa kwamba uthibitisho wao sasa ufanyike na kwamba kundi lishiriki sakramenti pamoja. Wakati akienda kuchukua divai kwa ajili ya sakramenti, Joseph alisimamishwa na malaika. Ni nini malaika alichomfundisha kuhusu sakramenti? (ona Mafundisho na Maagano 27:1–4).

Mistari hii inakufundisha nini kuhusu jinsi Mwokozi anavyokutaka wewe kuikaribia sakramenti? Unahisi umetiwa msukumo kufanya nini kwa sababu ya kile unachojifunza ?

mkate wa sakramenti na kikombe

Sakramenti inatukumbusha juu ya dhabihu ya Mwokozi.

Mafundisho na Maagano 27:15–18

Silaha za Mungu zitanisaidia kujilinda dhidi ya uovu.

Rais M. Russell Ballard alisema: “Hakuna hata kitu kimoja kilicho kikuu na muhimu tunachoweza kufanya kujilinda wenyewe kiroho. Nguvu ya kweli ya kiroho ipo katika vitendo kadhaa vidogo sana vilivyofumwa pamoja katika kitambaa cha kiroho kilichoimarishwa ambacho kinalinda na kukinga kutoka uovu wote” (“Kuwa Imara katika Bwana,” Ensign, Julai 2004, 8).

Unaposoma Mafundisho na Maagano 27:15–18, ungeweza kutengeneza chati kama hiyo iliyopo hapa chini. Unafanya nini kuvaa kila kipande cha silaha za Mungu?

Kipande cha silaha

Sehemu ya mwili imelindwa

Ni sehemu gani ya mwili inaweza kuwakilisha

Dirii ya haki

Moyo

Matamanio yetu na tabia ya huba

Chepeo ya wokovu

Kichwa au akili

Ona pia Waefeso 6:11–18; 2 Nefi 1:23.

Mafundisho na Maagano 28

Nabii aliye hai ndiye msemaji wa Mungu kwa ajili ya Kanisa Lake.

Fikiria vile ambavyo ingekuwa kama yoyote angeweza kupokea amri na ufunuo kwa ajili ya Kanisa lote. Wakati Hiram Page alipodai kuwa amepokea ufunuo kama ule, kulikuwa na ghasia miongoni mwa waumini wa Kanisa. Katika Mafundisho na Maagano 28, Bwana alifunua utaratibu kwa ajili ya ufunuo katika Kanisa Lake. Unajifunza nini kutoka sehemu hii kuhusu wajibu maalumu wa Rais wa Kanisa? Unajifunza nini kutoka kwenye maneno ya Bwana kwa Oliver Cowdery katika mstari wa 3? Unajifunza nini kutoka sehemu hii kuhusu jinsi Mungu anavyoweza kukuelekeza?

Ona pia Dallin H. Oaks, “Mistari Miwili ya Mawasiliano,” Ensign au Liahona, Nov. 2010, 83–86.

Mafundisho na Maagano 28:8–9

Kwa nini misheni ya Oliver Cowdery kwa Walamani ilikuwa muhimu?

Kusudi moja la Kitabu cha Mormoni ni “kwamba Walamani waweze kuja katika ufahamu wa baba zao, na kwamba waweze kujua ahadi za Bwana” (Mafundisho na Maagano 3:20). Hii ilikuwa kulingana na ahadi Bwana alizofanya kwa manabii wengi wa Kitabu cha Mormoni (ona, kwa mfano, 1 Nefi 13:34–41; Enoshi 1:11–18; Helamani 15:12–13). Waumini wa mwanzo wa Kanisa waliwafikiria Wahindi wa Amerika kuwa ni wa ukoo wa watu wa Kitabu cha Mormoni. (Msimamo rasmi wa Kanisa leo ni kwamba Walamani “ni miongoni mwa mababu wa wahindi wa Amerika” [Dibaji ya Kitabu cha Mormoni].)

Kusoma zaidi kuhusu misheni ya Oliver kwa makabila ya wahindi wa Amerika waliokuwa karibu yao, ona “Misheni kwa Walamani” (Funuo katika Muktadha, 45–49. Je, misheni hii inakufundisha nini kuhusu Bwana na kazi Yake?

ikoni ya kujifunza kifamilia

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko Kifamilia na Jioni ya Familia Nyumbani

Mafundisho na Maagano 27:1–2.Ni kwa jinsi gani tunaweza kukumbuka vyema dhabihu ya Mwokozi kwa ajili yetu tunaposhiriki sakramenti?

Mafundisho na Maagano 27:5–14.Tunajua nini kuhusu manabii katika mistari hii? Ungeweza kuchunguza kwa ajili ya taarifa kuwahusu katika Mwongozo wa Maandiko (scriptures.ChurchofJesusChrist.org). Ni baraka gani zimefunguliwa kwa ajili yetu kupitia funguo walizozishika? Kwa maelezo zaidi kuhusu baadhi ya funguo hizi, ona Mathayo 16:16–19; Mafundisho na Maagano 110:11–16.

Mafundisho na Maagano 27:15–18.Pengine familia yako ingefurahia kuigiza vita ya kujifanya na mavazi ya ziada kuwakilisha silaha za Mungu, kama vile kofia, fulana, aproni na viatu. Ni kwa jinsi gani silaha zinasaidia kutulinda katika vita? Jadilini baadhi ya athari za uovu familia yako inazokabiliana nazo na vitu mnavyoweza kufanya kuvaa silaha za kiroho. Fikiria kuonesha video “Vaeni Silaha Zote za Mungu” (ChurchofJesusChrist.org).

Mafundisho na Maagano 28:2–7.Tunajifunza nini kutoka kwenye mistari hii kuhusu wito wa nabii? Pengine wanafamilia wangeweza kupitia upya jumbe zilizopita kutoka kwa nabii wetu anaeishi na kushiriki jinsi ushauri wake unavyotusaidia kumfuata Yesu Kristo.

Mafundisho na Maagano 28:11.Tunapotaka kutoa sahihisho kwa mtu fulani, kwa nini ni muhimu kulishughulikia “kati yake na wewe peke yenu”?

Kwa mawazo zaidi kwa ajili ya kuwafundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Msingi.

Wimbo uliopendekezwa: “Njoo, Usikie Sauti ya Nabii,” Nyimbo za Kanisa, na. 21.

Kuboresha Kujifunza Kibinafsi

Jifunze maneno ya manabii na mitume wa siku za mwisho. Soma kile ambacho manabii na mitume wa siku za mwisho wamefundisha kuhusu kanuni unazopata ndani ya maandiko. Fikiria kupitia upya kielezo cha mada za mkutano mkuu kwenye conference.ChurchofJesusChrist.org au kwenye app ya Maktaba ya Injili.