Mafundisho na Maagano 2021
Machi 15–21. Mafundisho na Maagano 27–28: “Mambo Yote Lazima Yatendeke kwa Mpangilio”


“Machi 15–21. Mafundisho na Maagano 27–28: ‘Mambo Yote Lazima Yatendeke kwa Mpangilio,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)

“Machi 15–21. Mafundisho na Maagano 27–28,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2021

Joseph Smith

Machi 15–21

Mafundisho na Maagano 27–28

“Mambo Yote Lazima Yatendeke kwa Mpangilio”

Kweli zilizofundishwa katika Mafundisho na Maagano 27–28 zinaweza kuimarisha shuhuda za watoto unaowafundisha. Pale unapofikiria mahitaji ya watoto, ni kweli zipi umevutiwa kuzifokasia darasani?

Andika Misukumo Yako

ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Onesha picha ya nabii Joseph Smith na picha ya nabii wa sasa. Waalike watoto kuwataja watu katika picha na kushiriki mambo ambayo manabii hufanya.

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Mafundisho na Maagano 27:1–2

Sakramenti inanisaidia kumkumbuka Yesu Kristo.

Watoto wadogo wanaweza kujifunza umuhimu wa sakramenti na kutafuta njia za kumkumbuka Mwokozi wakati wa ibada hii takatifu.

Shughuli za Yakini

  • Waoneshe watoto picha ya Yesu akitoa sakramenti kwa Mitume Wake (ona Kitabu cha Sanaa ya Injili, na. 54). Inaweza kuwa ya namna gani kupokea sakramenti pamoja na Mwokozi? (ona Mafundisho na Maagano 27:5). Soma Mafundisho na Maagano 27:2, ukianza na “mkikumbuka kwa Baba,” na waombe watoto wasikilize kile Mwokozi anachotaka tukumbuke wakati tunapopokea sakramenti.

  • Waoneshe watoto mkate na maji na picha ya Mwokozi. Waache watoto washikilie picha wakati unapowafundisha kwamba sakramenti hutusaidia kumkumbuka Yesu Kristo.

  • Wasaidie watoto kufikiria juu ya mambo wanayoweza kufanya ili kumkumbuka Yesu wakati wa sakramenti. Ni nini familia zao hufanya kumsaidia kila mmoja kuwa mnyenyekevu? Waalike watoto kuchora picha wanayoweza kutazama wakati wa sakramenti ili kuwasaidia kumkumbuka Mwokozi.

Mafundisho na Maagano 27:15–18

Silaha za Mungu hunilinda mimi.

Fikiria juu ya jinsi unavyoweza kuwasaidia watoto unaowafundisha kuona jinsi kutii amri kulivyo sawa na kuvaa silaha za Mungu.

Shughuli za Yakini

  • Onesha picha ya deraya (ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia. Unaposoma Mafundisho na Maagano 27:15–18, wasaidie watoto kutafuta vipande vya deraya kwenye picha. Waambie watoto jinsi silaha za Mungu zilivyokusaidia “kushinda siku ya uovu” (mstari wa 15).

  • Muhtasari wa Waefeso katika Njoo Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano Jipya 2019 una ukurasa wa shughuli kuhusu silaha za Mungu. Kata vipande vya deraya, na waache watoto kuviweka juu ya mojawapo ya michoro wakati unaposoma Mafundisho na Maagano 27:15–18. Wasaidie watoto kuelewa mambo wanayoweza kufanya ili kuvaa silaha za Mungu, kama vile kuomba, kuchagua mema, kuwatumikia wengine, na kadhalika.

    watoto wakicheza

    Ninaweza kuvaa silaha za Mungu.

Mafundisho na Maagano 28:2, 6–7

Nabii anaongoza Kanisa

Je, watoto unaowafundisha wanajua kwa nini tunao manabii? Tumia Mafundisho na Maagano 28 ili kuwasaidia kujua kwamba nabii ni mtu pekee anayeweza kuliongoza Kanisa.

Shughuli za Yakini

  • Soma au simulia kwa maneno yako mwenyewe tukio la Hiram Page (ona “Sura ya 14: Nabii na Ufunuo kwa ajili ya Kanisa,” Hadithi za Mafundisho na Maagano, 56–57). Shiriki ushuhuda wako kwamba Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo walimchagua Joseph Smith kuongoza Kanisa katika siku yake (ona Mafundisho na Maagano 28:2). Shiriki ushuhuda wako kwamba nabii wa sasa ameitwa kumsaidia Bwana kuongoza Kanisa Lake katika siku yetu.

  • Waombe watoto kucheza “mfuate kiongozi”—mtoto mmoja angeweza kusimama mbele ya chumba, na watoto wengine wangeweza kuiga chochote anachofanya. Hii ingeweza kuongoza kwenye mjadala kuhusu kwa nini tunamfuata nabii. Ungeweza kuonesha picha ya Yesu Kristo na kusisitiza kwamba tunamfuata nabii kwa sababu yeye anamfuata Mwokozi na anazungumza maneno ya Mwokozi.

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Mafundisho na Maagano 27:1–2

Sakramenti inanisaidia kumkumbuka Yesu Kristo.

Ni kwa jinsi gani kujifunza kuhusu kanuni katika Mafundisho na Maagano 27:1–2 huwasaidia watoto unaowafundisha kuwa na uzoefu wenye maana kupokea sakramenti?

Shughuli za Yakini

  • Waalike watoto waandike mambo wanayodhani Mwokozi angetaka wajue kuhusu sakramenti. Ikihitajika, wangeweza kusoma “Sakramenti” katika Mwongozo kwenye Maandiko (scriptures.ChurchofJesusChrist.org). Waache wao washiriki baadhi ya mambo waliyoandika, na waombe waongeze kwenye orodha yao baada ya kusoma Mafundisho na Maagano 27:1–2. Ni kwa jinsi gani mambo katika orodha yao yataathiri jinsi wanavyopokea sakramenti kila Jumapili?

  • Wasaidie watoto kufikiria kuhusu kile inachomaanisha kupokea sakramenti “jicho likiwa kwenye utukufu wa [Mungu]” (mstari wa 2). Jadili maswali sawa na yafuatayo: Ni nini baadhi ya vivuta mawazo macho yetu au akili zetu zingeweza kufokasia wakati wa sakramenti? Nini tunaweza kufanya ili kufokasi umakini wetu kwa Mwokozi wakati tunapopokea sakramenti? Ni kwa jinsi gani hii hutusaidia kumfuata Yeye kila siku?

Mafundisho na Maagano 27:15–18

Silaha za Mungu hunisaidia kushinda uovu.

Watoto unaowafundisha watakabiliana na ushawishi mwingi wa uovu kote katika maisha yao. Baba wa Mbinguni anataka kuwasaidia kushinda uovu. Ni kwa jinsi gani unaweza kuwashawishi kuvaa silaha za Mungu?

Shughuli za Yakini

  • Waalike watoto wasome Mafundisho na Maagano 27:15–18 na kuchora vipande vya deraya vilivyotajwa (ikihitajika, wanaweza kurejelea mchoro kwenye muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia). Ni nini maneno yanayoelezea kila kipande cha deraya hutufundisha kuhusu kile tunachohitaji ili kupigana dhidi ya uovu unaotuzunguka (kwa mfano, haki, imani, wokovu, na kadhalika)?

  • Waalike watoto kufikiria mambo wanayoweza kufanya ili kushinda majaribu yanayowazunguka. Waombe wamalizie sentensi “Tunavaa silaha za Mungu kila siku kwa …” kwa kutumia mawazo yao. Wasaidie kuona jinsi juhudi zao za kuja kwa Kristo zinavyowasaidia kuvaa silaha za Mungu.

Mafundisho na Maagano 28:1–7, 15

Baba wa Mbinguni huniongoza kupitia Roho Mtakatifu.

Mafundisho na Maagano 28:1–7, 15 inaweza kuwasaidia watoto unaowafundisha kuelewa kwamba kila mmoja anaweza kuongozwa na Roho Mtakatifu, lakini ufunuo kwa ajili ya Kanisa daima utatolewa kupitia nabii.

Shughuli za Yakini

ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Waalike watoto kuwauliza wazazi wao ikiwa wanaweza kufundisha somo la jioni ya familia nyumbani juu ya jambo walilojifunza darasani.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Tumia muziki. Nyimbo za msingi na nyimbo za kanisa zinaweza kuwasaidia watoto wa rika zote kuelewa na kukumbuka kweli za injili katika njia isiyosahaulika. Zinaweza pia kuwafanya watoto kujihusisha kwa uchangamfu katika kujifunza.