Mafundisho na Maagano 2021
Machi 1–7. Mafundisho na Maagano 20–22 : “Kuinuka kwa Kanisa la Kristo”


“Machi 1–7. Mafundisho na Maagano 20–22 : ‘Kuinuka kwa Kanisa la Kristo,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)

“Machi 1–7. Mafundisho na Maagano 20–22,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2021

Nyumba ya Peter Whitmer

Nyumba ya Peter Whitmer, na Al Rounds

Machi 1–7

Mafundisho na Maagano 20–22

“Kuinuka kwa Kanisa la Kristo”

Unaposoma Mafundisho na Maagano 20–22 wiki hii, mawazo ya kufundisha yanaweza kukujia. Unaweza kupata mawazo ya ziada ya kufundishia katika muhtasari huu.

Andika Misukumo Yako

ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Onesha picha katika muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia, na waalike watoto kushiriki kile wanachojua kuhusu mpangilio wa Kanisa. Kwa msaada, ona “Sura ya 9: Kuundwa kwa Kanisa la Yesu Kristo” (Hadithi za Mafundisho na Maagano, 40–42).

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Mafundisho na Maagano 20–21

Kanisa la Yesu Kristo limerejeshwa.

Mnamo Aprili 6, 1830, Joseph Smith na Oliver Cowdery walikusanyika pamoja na wengine kuunda Kanisa lililorejeshwa la Yesu Kristo. Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia watoto unaowafundisha kuelewa umuhimu wa tukio hili?

Shughuli za Yakini

  • Tumia kichwa cha habari cha sehemu ya Mafundisho na Maagano 21 au sura ya 9 ya Hadithi za Mafundisho na Maagano kwa ufupi kuwaambia watoto kile kilichotokea siku Kanisa lilipoundwa. Ili kuwasaidia kuelewa tukio hili, onesha video “Kuundwa kwa Kanisa” (ChurchofJesusChrist.org).

  • Waambie watoto kwa nini una shukrani kwamba tuna Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho. Elezea kwamba kuwa muumini wa Kanisa kunatuandaa sisi kuishi na Mungu tena. Wasaidie kurudia kirai “mimi ni wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho” mara kadhaa au waimbe “The Church of Jesus Christ” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 77).

Mafundisho na Maagano 20:37, 71–74

Ninajitayarisha kubatizwa

Watoto unaowafundisha wanajitayarisha kwa ubatizo. Wasaidie kuelewa kile inachomaanisha kubatizwa na kile wanachoweza kufanya ili kuwa tayari.

Shughuli za Yakini

  • Onesha picha ya mtoto akibatizwa (ona Kitabu cha Sanaa ya Injili, na.104), na waombe watoto waoneshe vitu wanavyogundua. Soma au fanyia ufupisho Mafundisho na Maagano 20:71–74, na wasaidie watoto kuona jinsi picha inavyolandana na maelekezo katika mistari hii. Shuhudia kwamba tunapaswa kufuata mfano wa Mwokozi na kubatizwa katika njia ambayo Yeye ameamuru.

  • Fanyia ufupisho Mafundisho na Maagano 20:37. Je, tunajifunza nini kutoka katika mstari huu kuhusu watu wanaotaka kubatizwa? Onesha picha ya jinsi watoto wanavyoweza kujitayarisha kwa ajili ya ubatizo, kama vile kuwatumikia wengine na kuomba.

  • Imbeni wimbo kuhusu ubatizo, kama vile “When I Am Baptized”” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto103), au angalieni “The Baptism of Jesus” (biblevideos.ChurchofJesusChrist.org). Waalike watoto kushiriki hisia zao kuhusu kubatizwa.

Mafundisho na Maagano 20:75–79

Sakramenti hunisaidia kumkumbuka Yesu Kristo.

Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia watoto kuelewa vizuri zaidi kwa nini tunapokea sakramenti kila wiki?

Shughuli za Yakini

  • Wasomee watoto Mafundisho na Maagano 20:77. Waombe wanyanyuke wanaposikia kile tunachopaswa kukumbuka tunapokula mkate wa sakramenti. Fanya vivyo hivyo kwa mstari wa 79. (Unaweza kutaka kuonesha kuwa tunakunywa maji badala ya divai.) Ni kwa jinsi gani tunaweza kuonesha kwamba tunamkumbuka Yesu?

  • Waambie watoto kuhusu wakati ambapo ulifanya ahadi na kuishika. Waalike wasimulie hadithi sawa na hizo za kwao wenyewe. Elezea kwamba wakati tunapopokea sakramenti, tunafanya ahadi. Soma Mafundisho na Maagano 20:77, ukisisitiza ahadi tunazofanya za “daima kumkumbuka” na “kushika amri zake.” Waalike watoto washiriki wakati walipomkumbuka Mwokozi au kutii amri.

    watoto wakipokea sakramenti

    Sakramenti hunikumbusha kumfikiria Yesu Kristo.

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Mafundisho na Maagano 20–21

Kanisa la Yesu Kristo limerejeshwa.

Katika kutii agizo la Bwana, Joseph Smith, Oliver Cowdery, pamoja na wengine waliunda Kanisa lililorejeshwa la Yesu Kristo mnamo Aprili 6, 1830. Fikiria njia za kuwasaidia watoto kuona jinsi tukio hili lilivyobariki maisha yao.

Shughuli za Yakini

  • Wakumbushe watoto juu ya baadhi ya matukio ambayo wamekuwa wakijifunza kuyahusu—kama vile urejesho wa ukuhani na tafsiri ya Kitabu cha Mormoni. Kwa nini mambo haya yalihitaji kutokea kabla ya Kanisa kuundwa?

  • Onesha picha za mambo tunayofanya Kanisani ambayo yameelezewa katika sehemu ya 20, kama vile kujifunza kuhusu Mungu na Yesu Kristo, kuhudumu, kubatiza, na kupokea sakramenti. Wasaidie watoto kuoanisha picha hizi na maandiko ambayo yanazielezea, kama vile Mafundisho na Maagano 20:17–21, 47, 70, 72–74, 75–79, na kichwa cha habari cha sehemu ya 21. Ni baraka zipi tumepokea kwa sababu sisi ni waumini wa Kanisa?

  • Imbeni pamoja “The Church of Jesus Christ,” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 77).

Mafundisho na Maagano 20:37, 77, 79

Wakati nilipobatizwa, niliahidi kumfuata Yesu Kristo.

Wengi wa watoto katika darasa lako wamebatizwa. Wakumbushe juu ya agano walilofanya “kujichukulia juu yao jina la Yesu Kristo” (Mafundisho na Maagano 20:37).

Shughuli za Yakini

  • Waalike watoto wachache kuja wamejiandaa kushiriki kile walichohisi au uzoefu waliopata wakati walipobatizwa. Pengine wangeweza kuleta picha ya siku yao ya ubatizo ili kulionesha darasa. Kwa nini walichagua kubatizwa? Ni kwa jinsi gani kupokea Roho Mtakatifu kumewabariki?

  • Someni pamoja Mafundisho na Maagano 20:77, na waombe watoto watambue ahadi tunazofanya wakati wa sakramenti. Ili kuwasaidia watoto kuelewa kwamba kuna mambo tunayoweza kufanya kila siku ili “daima tumkumbuke” Yesu Kristo, mwalike mtoto mmoja kuigiza jambo analoweza kufanya ili kumkumbuka Mwokozi. Waombe watoto wengine kubashiri tendo hilo ni nini. Kulingana na mstari wa 77, ni kwa jinsi gani tunabarikiwa wakati daima tunapomkumbuka Mwokozi?

  • Wasaidie watoto kulinganisha Mafundisho na Maagano 20:37 na mstari wa 77 ili kupata kirai kinachojirudia kote. Waoneshe watoto kitu ambacho kina jina juu yake (kama vile jina la bidhaa au jina la mtu). Jina linatuambia nini kuhusu kitu? Someni pamoja Mafundisho na Maagano 20:37 ili kugundua ni jina la nani tunajichukulia juu yetu wakati tunapobatizwa. Je, inamaanisha nini kujichukulia jina la Yesu Kristo juu yetu? Ni kwa jinsi gani tunapaswa kufikiria na kutenda kwa sababu tunalo jina hili?

Mafundisho na Maagano 21:4–6

Ninabarikiwa pale ninapomfuata nabii.

Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia watoto kupokea baraka zilizoahidiwa katika mistari hii kwa wale wanaomfuata nabii?

Shughuli za Yakini

  • Andika ubaoni Amri na Baraka. Waalike watoto wasome Mafundisho na Maagano 21:4–6, wakitafuta amri Bwana alizotoa na baraka Alizoahidi. Waalike kuandika ubaoni kile wanachopata.

  • Onesha picha ya nabii wa sasa, na waalike watoto kushiriki jambo walilojifunza au kusikia kutoka kwake hivi karibuni. Someni pamoja Mafundisho na Maagano 21:5. Waalike watoto kuandika au kuchora jambo wanaloweza kufanya kumfuata nabii. Shiriki ushuhuda wako kwamba tunapomfuata nabii, tunamfuata Mwokozi.

ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Waalike watoto kutengeneza orodha ya sababu za kuwa na shukrani kwa Kanisa la Yesu Kristo lililorejeshwa. Wahimize kushiriki orodha yao pamoja na mwanafamilia au rafiki.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Tumia hadithi kufundisha mafundisho. “Hadithi huwasaidia watoto kuona jinsi ambavyo injili inatumika katika maisha ya kila siku. … Wakati unapofundisha watoto wadogo, panga njia za kuwashirikisha katika hadithi; kwa mfano, wanaweza kushikilia picha, kurudia maneno, au kuigiza vipengele” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 25) .