“Machi 22–28. Mafundisho na Maagano 29: ‘Yesu Kristo Atawakusanya Watu Wake,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)
“Machi 22–28. Mafundisho na Maagano 29,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi
Machi 22–28
Mafundisho na Maagano 29
Yesu Kristo Atawakusanya Watu Wake
Unawajua watoto unaowafundisha, na kuna kweli nyingi katika Mafundisho na Maagano 29 ambazo zinaweza kuwabariki. Fuata uvuvio wa Roho pale unaposoma sehemu ya 29, na weka kumbukumbu ya misukumo kuhusu jinsi utakavyofundisha watoto kweli hizi.
Andika Misukumo Yako
Alika Kushiriki
Fikiria kuwaalika watoto wachache kushiriki baadhi ya njia ambazo kwazo wanajifunza injili nyumbani—kibinafsi au na familia zao. Mualike mtoto mmoja au zaidi kushiriki ushuhuda wao wa jambo walilojifunza wiki hii nyumbani.
Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo
Yesu Kristo atakusanya watu wake kabla Yeye hajaja tena.
Tunakusanywa na Mwokozi pale tunapokubali na kufuata mafundisho Yake.
Shughuli za Yakini
-
Waache watoto wapake rangi ukurasa wa shughuli ya wiki hii wakati ukionesha video “Chicks and Hens” (ChurchofJesusChrist.org). Waombe watoto wasikilize ni jinsi gani kuku huwalinda vifaranga vyake.
-
Baada ya kusoma Mafundisho na Maagano 29:1–2, igizeni analojia ya Kristo akikusanya watu Wake “kama kuku avikusanyavyo vifaranga vyake.” Mtoto mmoja anaweza kujifanya kuwa kuku na kuchagua sehemu ya chumba na kusimama hapo. Wakati anapotoa “mlio wa kuku kuwaita vifaranga vyake,” wafanye watoto wote wakusanyike kumzunguka. Watoto wangeweza kufanya zamu kuwa kuku. Nyanyua juu picha ya Mwokozi na waalike watoto kukusanyika kumzunguka Yeye. Shiriki pamoja na watoto jinsi Yesu anavyotusaidia wakati tunapokusanyika kumzunguka.
Ninaweza kujiandaa kukutana na Mwokozi.
Siku moja, kila mmoja wetu atakuwa katika uwepo wa Yesu Kristo. Hali siku hiyo inaweza kuwa mbali hapo baadaye, watoto bado wanaweza kufikiria kuhusu vile itakavyokuwa na jinsi wanavyoweza kujiandaa kwa ajili ya hilo.
Shughuli za Yakini
-
Onesha picha ya Ujio wa Pili (ona Kitabu cha Sanaa ya Injili, na. 66), na muombe mtoto asome Mafundisho na Maagano 29:11. Wasaidie watoto kugundua virai katika maandiko ambavyo vinaelezea kile wanachoona katika picha. Shiriki pamoja na watoto jinsi unavyohisi kuhusu Ujio wa Yesu duniani tena.
-
Kama darasa, imbeni wimbo kuhusu Ujio wa Pili, kama vile “When He Comes Again”” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 82–83). Waoneshe watoto picha za vitu wanavyoweza kufanya ili kujiandaa kukutana na Mwokozi na kuishi pamoja Naye milele (ona Kitabu cha Sanaa ya Injili kwa ajili ya baadhi ya mawazo). Wasaidie kupata njia zingine za kujiandaa katika Mafundisho na Maagano 29:2–10.
Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa
Baba wa Mbinguni alitayarisha mpango wa wokovu kwa ajili yangu.
Kadiri mtoto anavyojua zaidi kuhusu mpango wa Mungu wa wokovu, ndivyo zaidi anavyoweza kufanya imani katika Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo ili kufuata mpango huo. Ni sehemu ipi ya mpango unahisi kuvutiwa kuifokasia?
Shughuli za Yakini
-
Waombe watoto kadhaa kushiriki mfano wa wakati ambapo walikuwa na mpango, kama vile kwa ajili ya safari au kwa ajili ya kukamilisha jukumu. Ungeweza pia kushiriki mifano ya mipango, kama vile kalenda yenye shughuli zilizoandikwa juu yake au maelekezo ya kutengeneza kitu. Kwa nini mipango ni muhimu? Shiriki pamoja na watoto kwamba Baba wa Mbinguni ana mpango ambao utaturuhusu sisi kuwa kama Yeye.
-
Ili kuwasaidia watoto kuelewa mpango wa Mungu, tengeneza alama zenye maneno haya: maisha kabla ya kuja duniani, Uumbaji, Anguko, maisha ya duniani, na Ujio wa pili. Baada ya kuelezea kila neno (ona Mafundisho na Maagano 29:9–45), toa kila alama kwa mtoto fotauti, na waombe wasimame katika mstari katika mpangilio sahihi ili kuonesha wakati gani kila tukio linatokea katika mpango wa Baba wa Mbinguni. Kila mtoto angeweza kushiriki kile anachojua kuhusu nini kiko katika alama yake. Wasaidie watoto kuona jinsi kujua mpango wa Baba wa Mbinguni hutusaidia kuwa zaidi kama Yeye na Mwokozi.
-
Tumia shughuli moja au zaidi hapo chini kufundisha kweli kuhusu mpango na jinsi zinavyotumika kwetu. Fikiria kuwaomba watoto kadhaa kuja wamejiandaa kukusaidia kufundisha.
-
Haki ya Kujiamulia. Wasaidie watoto kuelewa kwamba Baba wa Mbinguni ametupatia zawadi ya haki ya kujiamulia—uhuru wa kuchagua—na anatuwajibisha kwa chaguzi zetu (ona Mafundisho na Maagano 29:39–40). Tengeneza alama mbili kwa ajili ya kila mtoto: moja ambayo huwakilisha kufanya uchaguzi mzuri (kwa mfano, uso wa furaha) na moja ambayo huwakilisha uchaguzi mbaya (kwa mfano, uso wa kununa). Shiriki mifano ya chaguzi nzuri na chaguzi mbaya, na waombe watoto kuinua alama sahihi. Waombe watoto kushiriki baraka ambazo huja wakati tunapomfuata Yesu Kristo. Kwa nini Baba wa Mbinguni hutuacha tufanye chaguzi zetu wenyewe?
-
Amri. Waalike watoto kutengeneza orodha ubaoni ya baadhi ya amri. (Kwa mfano, wangeweza kutafuta Kutoka 20:3–17 na Kitabu cha Sanaa ya Injili, 103–15.) Kwa nini Baba wa Mbinguni anatupatia amri? Ni nini tunajifunza kutoka katika Mafundisho na Maagano 29:35 kuhusu amri za Baba wa Mbinguni?
-
Upatanisho wa Yesu Kristo. Wasaidie watoto kuona kwamba Baba wa Mbinguni aliandaa njia kwa ajili yetu kusamehewa pale tunapofanya chaguzi mbaya. Muombe kila mtoto kusoma mojawapo ya mistari katika Mafundisho na Maagano 29:1, 42–43 na kushiriki kile inachofundisha kuhusu Upatanisho wa Mwokozi. Tafuta njia ya ubunifu kuwaalika watoto kushiriki kile walichopata, kama katika mpangilio wa siku zao za kuzaliwa, au kimo mfupi hadi mrefu, na kadhalika.
-
Yesu Kristo atakusanya watu wake kabla Yeye hajaja tena.
Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia watoto unaowafundisha kufurahia kuhusu kusaidia kukusanya Israeli?
Shughuli za Yakini
-
Waalike watoto wasome Mafundisho na Maagano 29:1–2 na kutafuta kile Bwana Alichojifananisha nacho. Ni nini watoto hufikiria wakati wanaposoma mlinganisho huu? Ni nini Bwana anasema sharti tufanye ili tukusanywe na Yeye?
-
Njia moja ya kuwafanya watoto wawe na shauku kuhusu kukusanyika ni kushiriki hadithi ya mtu ambaye amejiunga na Kanisa. Kwa mfano, nani aliitambulisha familia yako Kanisani? Fikiria kuwaomba watoto mapema kutafuta kuhusu muumini wa kwanza wa Kanisa kwenye familia yako na kushiriki hadithi yake pamoja na darasa.
-
Waalike watoto kutengeneza orodha ya njia wanazoweza kusaidia watu kukusanyika kwa Mwokozi. Kwa mfano, wangeweza kuwaalika marafiki au wanafamilia kwenye shughuli ya Msingi au jioni ya familia pamoja na familia zao.
-
Makala ya imani ya kumi inazungumza kuhusu kukusanyika kwa Israeli. Je, kuna yeyote kati ya watoto aliyekariri makala hii ya imani? Ikiwa ndivyo, waalike kuikariri kwa darasa. Ikiwa sivyo, wasaidie kuweka lengo la kuikariri.
Himiza Kujifunza Nyumbani
Waalike watoto waandike ukweli waliojifunza darasani. Omba mawazo kadhaa juu ya kile watakachofanya kushiriki ukweli huu pamoja na familia zao.