Mafundisho na Maagano 2021
Machi 8–14. Mafundisho na Maagano 23–26: “Kuimarisha Kanisa”


“Machi 8–14. Mafundisho na Maagano 23–26: ‘Kuimarisha Kanisa,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)

“Machi 8–14. Mafundisho na Maagano 23–26,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2021

Picha
Emma Smith

Machi 8–14

Mafundisho na Maagano 23–26

“Kuimarisha Kanisa”

Wakati unapojiandaa kufundisha, fikiria mawazo ya shughuli kote katika sehemu ya “Watoto Wadogo” na “Watoto Wakubwa”.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Onesha picha ya Emma Smith (ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo Unifuate—Kwa ajili ya Watu Binafsi na Familia.). Waalike watoto kushiriki kile wanachofahamu kuhusu Emma, ikijumuisha mambo wanayoweza kuwa wamejifunza wakati wakisoma Mafundisho na Maagano 25 wiki hii iliyopita. “Sura ya 13: Joseph na Emma”(Hadithi za Mafundisho na Maagano, 51–55) zinaweza kusaidia.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Mafundisho na Maagano 23:6; 26:1.

Mungu ananitaka niombe na kujifunza kutoka kwenye maandiko kila siku.

Bwana aliwashauri viongozi wa mwanzo na marafiki wa Kanisa kuomba (ona Mafundisho na Maagano 23:6) na kujifunza maandiko (ona Mafundisho na Maagano 26:1). Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia watoto kufanya maombi na kujifunza maandiko kuwa sehemu ya maisha yao?

Shughuli za Yakini

  • Wasomee watoto kutoka Mafundisho na Maagano 23:6, ukianza na “ni lazima uombe.” Wasaidie kutambua njia tofauti na sehemu tofauti ambazo kwazo Bwana amesema tunapaswa kuomba. Waalike wachore picha zao wenyewe wakiomba katika mojawapo ya njia hizo na sehemu hizo.

  • Kama itahitajika, waelezee watoto jinsi ya kuomba. Wimbo kuhusu kuomba, kama “I Pray in Faith” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 14), unaweza kusaidia.

  • Wasomee watoto, “Muda wenu na utumike kwa kujifunza maandiko” (Mafundisho na Maagano 26:1). Waambie kwa nini unajifunza maandiko. Wasaidie wafikirie jinsi wanavyoweza kujifunza kutoka kwenye maandiko, hata kama bado hawawezi kusoma.

  • Imbeni pamoja “Search, Ponder, and Pray” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 109) au wimbo mwingine kuhusu maombi na kujifunza maandiko. Wasaidie watoto kugundua baraka zilizoahidiwa katika wimbo. Waambie kuhusu hisia za kiroho ambazo umewahi kuwa nazo wakati ukiomba na kusoma maandiko.

Mafundisho na Maagano 25:11–12

Yesu hupenda “nyimbo za moyoni.”

Bwana alisema kwamba muziki mtakatifu “unanipendeza mimi.” Wasaidie watoto kuona kuimba kama si tu shughuli ya kufurahisha bali pia njia ya kumwabudu Yeye.

Shughuli za Yakini

  • Mwalike kila mtoto ashiriki wimbo wa kanisa anaoupenda sana, na imbeni baadhi ya nyimbo hizo pamoja. Wasomee watoto Mafundisho na Maagano 25:12, na waalike wafikirie jinsi Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo wanavyohisi wakati wanapotusikia tukiimba nyimbo hizi.

  • Wafundishe watoto wimbo kuhusu kuimba, kama vile “Lift Up Your Voice and Sing” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 252), au wimbo kuhusu Yesu Kristo kama vile “He Sent His Son” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 34–35). Waalike waimbe wimbo pamoja na familia zao wiki hii.

    Picha
    watoto wakiimba

    Kuimba ni njia moja tunayoweza kuonesha upendo wetu kwa Mungu.

Mafundisho na Maagano 25:13,15

Ninaweza kujiandaa kufanya maagano matakatifu.

Watoto unaowafundisha wanajiandaa kufanya maagano yao ya kwanza na Baba wa Mbinguni wakati wanapobatizwa. Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia kuona jinsi maagano yetu yalivyo ya thamani?

Shughuli za Yakini

  • Wasomee watoto Mafundisho na Maagano 25:13. Elezea kwamba neno “uyashike” katika mstari huu linamaanisha kung’ang’ania kitu kwa nguvu. Ili kuwasaidia kuelewa, pitisha kitu kigumu, kama vile jiwe (au hata fimbo ya chuma), kuzunguka chumba na waalike watoto kushikilia kitu kile kwa nguvu kadiri wawezavyo. Elezea kwamba kushika maagano yetu kunamaanisha kung’ang’ania (au kutunza) ahadi tunazofanya na Baba wa Mbinguni na kutoyaacha (au kutokata tamaa).

  • Tumia ukurasa wa shughuli ya wiki hii kuwafundisha watoto kuhusu nyakati tunapofanya maagano na Baba wa Mbinguni. Soma Mafundisho na Maagano 25:15, na uelezee kwamba “taji la haki” huwakilisha baraka za kurudi kuishi na Mungu, Mfalme wetu wa Mbinguni.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Mafundisho na Maagano 23:3–7; 25:7

Yesu Kristo ananitaka niwaimarishe wale walio karibu nami.

Wakati Kanisa lilipoundwa mwanzo, hakukuwa na waumini wengi. Bwana aliwaomba Watakatifu kujenga Kanisa kwa kushiriki injili na kuimarishana kila mmoja. Tunaweza kufanya vivyo hivyo leo.

Shughuli za Yakini

  • Waombe watoto kutafuta kila mtajo wa maneno “kushawishi” na “shawishi” katika Mafundisho na Maagano 23:3–7; 25:7. Wasaidie kutoa maana za maneno haya. Ni kwa jinsi gani kumsihi mtu kunawaimarisha? Waalike watoto kuigiza “kushawishi” mtu lakini kufanya hivyo kwa upendo.

  • Ni kwa jinsi gani tunaweza kufanya vizuri zaidi katika kazi ya kuwaimarisha waumini wengine wa Kanisa? Ili kuelezea kwa mfano kanuni hii, mpe mtoto mmoja jukumu ambalo linahitaji wasaidizi wengi. Kisha waombe watoto wengine kusaidia, na kujadili ni rahisi kiasi gani jukumu limekuwa. Shiriki uzoefu ambapo uliimarishwa kwa huduma ya muumini mwenza wa Kanisa.

Mafundisho na Maagano 24: 1, 8

Mwokozi anaweza kuniinua “juu ya mateso [yangu].”

Joseph Smith aliteseka majaribu mengi, lakini aliweza “kuwa mvumilivu katika mateso” kwa sababu Bwana aliahidi kwamba Yeye daima angekuwa pamoja naye.

Shughuli za Yakini

  • Wasaidie watoto kuorodhesha ubaoni baadhi ya mateso au changamoto ambazo Joseph Smith na Watakatifu wengine wa Mwanzo walizokuwa wakipata (ona “Sura ya 11: Watu Zaidi Wanajiunga na Kanisa,” Hadithi za Mafundisho na Maagano, 46–47, au video inayohusiana kwenye ChurchofJesusChrist.org). Kisha waalike kugundua kile ambacho Bwana alimwambia Joseph kuhusu mateso katika Mafundisho na Maagano 24:1, 8 Ni kwa jinsi gani tunaweza kutafuta msaada wa Mwokozi wakati tunapokuwa na wakati mgumu?

  • Ili kuwafundisha watoto kwamba wakati mwingine tunahitaji kuwa “wavumilivu katika mateso [yetu],” ungeweza kuonesha video “Continue in Patience” (ChurchofJesusChrist.org). Waombe watoto wafikirie kitu wanachotaka sana lakini wanapaswa kukisubiria. Kwa nini Bwana wakati mwingine anatuhitaji kuwa na uvumilivu kipindi cha nyakati za changamoto katika maisha yetu? Ni kwa jinsi gani Yeye hutujulisha kwamba “Yupo pamoja [nasi] wakati wa mateso yetu?

Mafundisho na Maagano 25:13

Ninaweza “kuyashikilia maagano” niliyofanya.

Punde baada ya Emma Smith kubatizwa, Bwana alimwambia, “Shikilia maagano ambayo umeyafanya.” Fikiria ni kwa jinsi gani ushauri huu ungeweza kuwabariki watoto unaowafundisha.

Shughuli za Yakini

  • Someni pamoja Mafundisho na Maagano 25:13, na uwaulize watoto kile inachomaanisha katika mstari huu “kuyashikilia maagano” tunayofanya. Ili kuelezea kwa mfano, pitisha vitu kwa mzunguko ambavyo vimefungwa imara pamoja na waruhusu watoto kujaribu kuvitenganisha. Kwa nini neno “shikilia” ni neno zuri kuelezea jinsi tunavyopaswa kuhisi kuhusu maagano yetu?

  • Ikihitajika, rejea pamoja na watoto maagano tunayofanya wakati tunapobatizwa (ona Mosia 18:8–10; Mafundisho na Maagano 20:37). Inamaanisha nini “kushikilia” maagano haya?

  • Pitieni pamoja baadhi ya kile mnachojua kuhusu maisha ya Emma Smith (ona “Sura ya 13: Joseph na Emma” [Hadithi za Mafundisho na Maagano, 51–55], au video inayohusiana kwenye ChurchofJesusChrist.org). Mpe kila mtoto mstari mmoja au miwili kutoka sehemu ya 25, na waalike kushiriki jinsi ushauri wa Bwana na jukumu vingeweza kumsaidia Emma “kuyashikilia maagano” aliyofanya. Ni kwa jinsi gani tunaweza kufuata mfano wake?

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Waalike watoto kuchagua mstari wanaoupenda ambao mliujadili pamoja, aandike rejeleo, na kushiriki pamoja na mwanafamilia au rafiki.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Himiza staha. Wasaidie watoto kuelewa kwamba kipengele muhimu cha staha ni kufikiria juu ya Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo. Ungeweza kuwakumbusha watoto kuwa wenye staha kwa kuimba wimbo kimya kimya au kimoyomoyo au kuonesha picha ya Yesu.

Chapisha