Mafundisho na Maagano 2021
Februari 22–28. Mafundisho na Maagano 18–19:, “Thamani ya Nafsi Ni Kubwa”


“Februari 22–28. Mafundisho na Maagano 18–19: ‘Thamani ya Nafsi Ni Kubwa,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)

“Februari 22–28. Mafundisho na Maagano 18–19,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2021

Picha
Shamba la Martin Harris

Shamba la Martin Harris, na Al Rounds

Februari 22–28

Mafundisho na Maagano 18–19

Thamani ya Nafsi Ni Kubwa.

Muombe Baba wa Mbinguni akusaidie kupata kanuni katika Mafundisho na Maagano 18–19 ambazo zitakuwa hasa zenye maana kwa watoto.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Soma Mafundisho na Maagano 18:2, na uelezee kwamba Roho alimsaidia Oliver Cowdery kujua kwamba maandiko ni ya kweli. Waambie watoto kuhusu uzoefu wakati Roho alipokushuhudia kwamba maandiko ni ya kweli. Waache washiriki uzoefu ambapo walihisi kwamba maandiko ni ya kweli.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Mafundisho na Maagano 18:10–12

Kila mmoja wetu ana thamani kubwa kwa Mungu.

Wakati watoto wanapojua kwamba Baba wa Mbinguni anawapenda wao—na watoto Wake wote—wanakuwa wenye ujasiri zaidi na wakarimu zaidi kwa wengine.

Shughuli za Yakini

  • Wasaidie watoto kurudia pamoja nawe Mafundisho na Maagano 18:10 mara kadhaa. Elezea kwamba “nafsi” humaanisha watoto wote wa Mungu. Rudia mstari wa 10 pamoja na watoto, wakati huu ukibadilisha “nafsi” kwa kuweka majina ya watoto. (Ona pia ukurasa wa shughuli ya wiki hii.)

  • Wasaidie watoto kufikiria vitu ambavyo watu huvipa thamani. Kisha waache watoto wachukue zamu kutazama kwenye kioo, na wanapofanya hivyo, mwambie kila mtoto kwamba yeye ni mtoto wa Mungu na ana thamani kubwa. Shuhudia kwamba kwa Baba wa Mbinguni, wana thamani kubwa kuliko vitu vyote walivyofikiria mwanzo.

Mafundisho na Maagano 6:13–16.

Kushiriki injili kunaleta shangwe kubwa.

Ni kwa jinsi gani utawashawishi watoto kuwaalika wengine kuja kwa Kristo na kupata uzoefu wa shangwe kubwa?

Shughuli za Yakini

  • Waambie watoto kuhusu jambo ambalo linakupa shangwe. Muache kila mtoto akuambie kuhusu jambo ambalo linampa shangwe. Soma Mafundisho na Maagano 18:13, 16. Nini kinampa Bwana shangwe? Ni nini ambacho anasema kitatupatia shangwe?

  • Imbeni pamoja wimbo kuhusu kazi ya umisionari, kama vile “I Want to Be a Missionary Now” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto,168), na wasaidie watoto kufikiria njia wanazoweza kushiriki injili, ikijumuisha nyumbani mwao wenyewe. Simulia juu ya wakati ambapo ulishiriki injili, na waache watoto washiriki uzoefu wao.

Mafundisho na Maagano 19:18–19, 23–24

Yesu Kristo alimtii Baba wa Mbinguni, hata wakati ilipokuwa vigumu.

Utayari wa Mwokozi “kunywa kikombe kichungu, na [kutosita]” (mstari wa 18) ni mfano kwetu sote wa kutii mapenzi ya Baba wa Mbinguni. Fikiria jinsi unavyoweza kuwapa msukumo watoto kufuata mfano wa Yesu.

Shughuli za Yakini

  • Onesha picha ya Yesu Kristo akiteseka Gethsemane (ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia). Waache watoto waseme kile wanachojua kuhusu kile kinachotendeka katika picha hii. Fupisha kwa maneno yako mwenyewe kile ambacho Mwokozi alisema katika Mafundisho na Maagano 19:18–19 kuhusu mateso Yake. Sisitiza kwamba kuteseka kwa ajili ya dhambi zetu lilikuwa ni jambo gumu kuliko yote ambayo yeyote amewahi kufanya, lakini kwa sababu Yesu alimpenda Baba Yake pamoja na sisi, Yeye alitii mapenzi ya Mungu. Ni kwa jinsi gani tunaweza kumtii Baba wa Mbinguni?

  • Wasaidie watoto kufikiria juu ya matendo madogo ambayo yanakwenda sambamba na virai katika Mafundisho na Maagano 19:23. Soma mstari mara kadhaa wakati watoto wakifanya matendo. Wasaidie wafikirie njia tunazoweza kujifunza juu ya Kristo na kusikiliza maneno Yake.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Mafundisho na Maagano 18:10–12

Kila mmoja wetu ana thamani kubwa kwa Mungu.

Watu wengi wanahangaika na hisia za kutokuwa na thamani; wengine si wakarimu kwa watu ambao wako tofauti nao. Ujumbe wenye nguvu wa Mafundisho na Maagano 18:10 unaweza kubadilisha jinsi tunavyojiangalia wenyewe pamoja na watu wanaotuzunguka.

Shughuli za Yakini

  • Muombe kila mtoto kuandika jina lake kwenye kipande cha karatasi na kupitisha karatasi kuzunguka darasa. Waalike waandike kwenye kila karatasi waliyopokea jambo wanalopenda kuhusu mtu yule. Watie moyo kuwa wakarimu na wenye kujali katika maoni yao. Kisha wasaidie watoto kusoma Mafundisho na Maagano 18:10–12, na waalike kushiriki kile wanachojifunza kuhusu jinsi Mungu anavyohisi kutuhusu sisi. Elezea kwamba sisi sote tuna thamani kubwa kwa Mungu kwa sababu sisi ni watoto Wake.

  • Waoneshe watoto kitu ambacho ni cha thamani kubwa kwako. Ni kwa jinsi gani tunavichukulia vitu ambavyo ni vya thamani kwetu. Muombe mtoto asome Mafundisho na Maagano 18:10. Ni kwa jinsi gani tunaweza kuwaonesha watu wengine kuwa “thamani ya nafsi [zao] ni kubwa” mbele zetu?

    Picha
    Yesu akiwa amembeba mvulana mdogo

    Thamani ya Nafsi, na Liz Lemon Swindle

Mafundisho na Maagano 19:16–19

Yesu Kristo aliteseka kwa ajili yangu.

Ni kwa jinsi gani utaalika roho ya staha katika darasa lako ili kwamba Roho Mtakatifu aweze kushuhudia kwa watoto kwamba Yesu Kristo alilipa gharama kwa ajili ya dhambi zao?

Shughuli za Yakini

  • Shiriki hadithi ya Yesu Kristo akiteseka kwa ajili ya dhambi zetu (ona “Sura ya 51: Yesu anateseka katika Bustani ya Gethsemane,” Hadithi za Agano Jipya, 129–32, au video inayohusiana kwenye ChurchofJesusChrist.org). Waalike watoto kusimulia hadithi tena kwa maneno yao wenyewe, na kisha waalike kusoma jinsi Mwokozi alivyoelezea uzoefu huu katika Mafundisho na Maagano 19:16–19. Ni nini tunajifunza kutokana na maelezo Yake?

  • Waalike watoto kufumba macho yao pale unaposoma Mafundisho na Maagano 19:16–19 na kufikiria kuhusu jinsi wanavyohisi kuhusu Mwokozi. Wasaidie watoto kutafuta katika Nyimbo za Kanisa au kwenye Kitabu cha Nyimbo za Watoto kwa ajili ya nyimbo ambazo zinawasaidia kuelezea hisia zao kuhusu Yesu Kristo (ona vielezo vya mada katika vitabu hivi). Waalike watoto kuimba nyimbo walizochagua na kutoa shuhuda zao.

  • Wasaidie watoto kukariri makala ya imani ya tatu.

Mafundisho na Maagano 19:26, 34–35, 38

Baraka za Mungu ni kuu kuliko hazina za duniani.

Kuchapisha Kitabu cha Mormoni ilikuwa gharama kubwa, na Joseph Smith hakuweza kukidhi hilo. Bwana alimwomba Martin Harris “kutoa sehemu ya mali [yake],” shamba lake lililostawi, ili kumlipa mchapishaji (mstari wa 34). Tumepokea baraka nzuri mno kwa sababu ya dhabihu za Martin na wengine wengi.

Shughuli za Yakini

  • Andika ubaoni maswali sawa na yafuatayo kuwasaidia watoto kuelewa Mafundisho na Maagano 19:26, 34–35, 38: ni nini Bwana alimwomba Martin Harris kufanya? Ni kwa nini Bwana alimuomba kufanya hilo? Ni nini Bwana aliahidi kama malipo? Waalike watoto kufanya kazi katika jozi ili kupata majibu katika mistari hii. Waulize jinsi ambavyo wangehisi kama wangekuwa Martin Harris.

  • Waoneshe watoto nakala ya Kitabu cha Mormoni, na waambie jambo unalopenda kuhusu kitabu hicho. Waalike kushiriki jinsi wanavyohisi kuhusu Kitabu cha Mormoni. Kwa ufupi zungumza kuhusu dhabihu ya Martin Harris ili Kitabu cha Mormoni kiweze kuchapishwa (Hadithi za Mafundisho na Maagano, 33). Ni nini Bwana alimwambia Martin katika Mafundisho na Maagano 19:38 ambacho kingeweza kumsaidia kuwa mwaminifu na mtiifu? Wasaidie watoto kufikiria juu ya kitu wanachoweza kutoa dhabihu ili kumtii Mungu au kusaidia katika kazi Yake.

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Waalike watoto kumfikiria mtu ambaye angeweza kusaidiwa na kile walichojifunza kutoka Mafundisho na Maagano 18 au 19—kwa mfano, kwamba sote tuna thamani kubwa kwa Mungu. Wahimize kupanga jinsi watakavyoshiriki kile walichojifunza pamoja na mtu yule.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Wasaidie watoto kujifunza kutoka kwenye maandiko. Baadhi ya watoto hupata wakati mgumu kusoma maandiko. Kufokasi kwenye mstari mmoja au kirai kunaweza kuwasaidia.

Chapisha