Mafundisho na Maagano 2021
Februari 8–14. Mafundisho na Maagano 12–13; Joseph Smith—Historia ya 1:66–75: “Juu Yenu Ninyi Watumishi Wenzangu”


“Februari 8–14. Mafundisho na Maagano 12–13; Joseph Smith—Historia ya 1:66–75: ‘Juu Yenu Ninyi Watumishi Wenzangu,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)

“Februari 8–14. Mafundisho na Maagano 12–13; Joseph Smith—Historia ya 1:66–75: “Juu Yenu Ninyi Watumishi Wenzangu,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2021

Picha
Mto Susquehanna

Februari 8–14

Mafundisho na Maagano 12–13; Joseph Smith—Historia ya 1:66–75.

“Juu Yenu Ninyi Watumishi Wenzangu”

Watoto unaowafundisha wanatoka katika hali tofauti na wana mahitaji tofauti. Unapojitayarisha, fikiria kuhusu jinsi unavyoweza kuwasaidia vyema kujifunza kweli zilizofundishwa katika Mafundisho na Maagano 12–13 na Joseph Smith—Historia ya 1:66–75.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Waalike watoto washiriki nyakati walipomuona mtu akibatizwa au kupokea baraka ya ukuhani. Ni kwa jinsi gani Joseph Smith na Oliver Cowdery walipokea ukuhani?

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Mafundisho na Maagano 13

Yohana Mbatizaji alirejesha Ukuhani wa Haruni.

Mnamo Mei 15,1829, Yohana Mbatizaji aliwatokea Joseph Smith na Oliver Cowdery na kuwapa funguo za Ukuhani wa Haruni. Ni kwa jinsi gani kujifunza kuhusu tukio hili kunawabariki watoto unaowafundisha?

Shughuli za Yakini

  • Waambie watoto kuhusu jinsi Ukuhani wa Haruni ulivyorejeshwa (ona Joseph Smith—Historia ya 1:68–70; ona pia “Sura ya 6: Joseph na Oliver Wanapewa Ukuhani,” Hadithi za Mafundisho na Maagano, 26–27). Au mwalike mwanaume katika kata kuja darasani na kusimulia hadithi kana kwamba alikuwa Yohana Mbatizaji, akiwasomea watoto kile Yohana alichomwambia Joseph Smith na Oliver Cowdery.

  • Onesha picha ya Yohana Mbatizaji akimbatiza Mwokozi na kurejesha Ukuhani wa Haruni (Kitabu cha Sanaa ya Injili, 35, 93; ona pia picha katika muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia). Waalike watoto kushiriki kile wanachojua kuhusu nini kinatokea katika picha (ona Mathayo 3:13–17; Mafundisho na Maagano 13; Joseph Smith—Historia ya 1:68–70).

  • Wasaidie watoto kujifunza wimbo kuhusu ukuhani, kama vile “The Priesthood Is Restored” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto,89). Waalike watoto kutembea kuzunguka nyumba pale wanapoimba, wakifanya zamu kushikilia picha kutoka muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia.

Mafundisho na Maagano 13

Ukuhani ni nguvu ya Mungu.

Masomo kuhusu urejesho wa Ukuhani wa Haruni ni nyakati kuu za kusaidia watoto kuelewa vizuri zaidi kile ukuhani unachomaanisha na jinsi unavyoweza kuwabariki.

Shughuli za Yakini

  • Leta vitu kadhaa darasani, ikijumuisha ufunguo. Onesha vitu hivyo, na waombe watoto kusikiliza pale unaposoma Mafundisho na Maagano 13 na kutafuta kitu ambacho kimetajwa katika maandiko. Tunaweza kufanya nini kwa kutumia ufunguo? Onesha picha ya mambo tunayoweza kufanya kwa sababu Ukuhani wa Haruni ulirejeshwa (ona ukurasa wa shughuli ya wiki hii; ona pia Kitabu cha Sanaa ya Injili, 103–4, 107–8). Waambie watoto jinsi ukuhani ulivyobariki maisha yako.

  • Ili kuwasaidia watoto kujifunza kirai Ukuhani ni nguvu ya Mungu, waombe wapige makofi pale wanaposema kila silabi. Onesha kifaa ambacho kinahitaji betri ili kufanya kazi, na fundisha kwamba, kama vile betri inavyoleta nguvu kwenye kifaa, ukuhani huleta nguvu ya Mungu katika maisha yetu. Shiriki ushuhuda wako juu ya baraka ambazo zimekuja kwako kwa sababu ya ukuhani.

Joseph Smith—Historia ya 1:66–75

Ninaweza kubatizwa.

Joseph Smith na Oliver Cowdery walisoma kuhusu ubatizo katika Kitabu cha Mormoni na walitaka kujua zaidi. Unaweza kuwasaidia watoto unaowafundisha kutazamia ubatizo wao na kujifunza zaidi kuhusu ibada hii takatifu.

Shughuli za Yakini

  • Onesha video “Urejesho wa Ukuhani wa Haruni” (ChurchofJesusChrist.org). Simamisha video mara kwa mara ili kuuliza watoto maswali kama vile “Kwa nini Joseph Smith na Oliver Cowdery walikwenda msituni?” na “Ni kwa jinsi gani unadhani Joseph Smith na Oliver Cowdery walihisi baada ya kubatizwa?” Waombe kushiriki jinsi wanavyodhani watahisi wakati wanapobatizwa.

  • Waambie watoto kuhusu Joseph Smith na Oliver Cowdery wakibatizwa (ona Joseph Smith—Historia ya 1:68–74; ona pia “Sura ya 6: Joseph na Oliver Wanapewa Ukuhani,” Hadithi za Mafundisho na Maagano, 26–28). Sisitiza shangwe Joseph na Oliver waliyohisi, na waambie watoto kuhusu ubatizo wako. Waalike wachore picha zao wenyewe wakiwa wanabatizwa siku moja.

    Picha
    mvulana akibatizwa

    Ninaweza kubatizwa kwa sababu ukuhani ulirejeshwa.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Mafundisho na Maagano 13; Joseph Smith—Historia ya 1:66–72

Yohana Mbatizaji alirejesha Ukuhani wa Haruni.

Maelezo ya urejesho wa Ukuhani wa Haruni yanaweza kuwasaidia watoto unaowafundisha kuelewa kweli muhimu kuhusu ukuhani na utawazo wa ukuhani.

Shughuli za Yakini

Mafundisho na Maagano 13

Ninapokea baraka kupitia Ukuhani wa Haruni.

Tunapokea baraka nyingi kupitia Ukuhani wa Haruni. Unaweza kufanya nini kuwasaidia watoto unaowafundisha kuelewa kwamba baraka hizi zinawezeshwa kwa sababu ukuhani ulirejeshwa?

Shughuli za Yakini

  • Weka picha ya ubatizo na sakramenti ndani ya chombo ambacho kinahitaji ufunguo ili kukifungua. Jadili kwa nini funguo ni muhimu, na waruhusu watoto kutumia ufunguo kufungua chombo. Waalike watoto wasome Mafundisho na Maagano 13, na tafuta maneno na virai ambavyo huwafundisha ni baraka zipi huja kutokana na Ukuhani wa Haruni.

  • Onesha video “Blessings of the Priesthood” (ChurchofJesusChrist.org), na waombe watoto kutambua njia ambazo watu katika video wanabarikiwa kwa sababu ya ukuhani.

Joseph Smith—Historia ya 1:73-74

Roho Mtakatifu anaweza kunisaidia kuelewa maandiko.

Baada ya Joseph Smith na Oliver Cowdery kubatizwa, Roho Mtakatifu aliwasaidia kuelewa maandiko vizuri zaidi. Hili linaweza kuwa la kutia moyo kwa watoto, ambao wanaweza kupata ugumu wa kuelewa maandiko.

Shughuli za Yakini

  • Leta chemsha bongo rahisi darasani, na waalike watoto kuliweka pamoja. Wakati wakifanya hilo, waulize jinsi kusoma maandiko kulivyo sawa na kuweka chemsha pamoja. Someni pamoja Joseph Smith—Historia ya 1:73–74, na waalike watoto kushiriki kile kilichomsaidia Joseph na Oliver kuelewa maandiko. Nini tunaweza kufanya kutafuta msaada wa Roho Mtakatifu pale tunapojifunza maandiko?

  • Waalike watoto kutengeneza alamisho ambalo wanaweza kuweka katika maandiko yao ili kuwakumbusha kutafuta msaada wa Roho Mtakatifu wakati wanaposoma. Pengine wangeweza kutafuta kirai chenye kutia msukumo katika Joseph Smith—Historia ya 1:74 ambacho wangeweza kuandika kwenye alamisho lao.

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Ikiwa huna muda kwa ajili ya watoto kumaliza ukurasa wa shughuli darasani, fikiria kutuma nakala nyumbani ili watoto waweze kuufanyia kazi pamoja na familia zao.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Kuwa mwepesi kubadilika na msikilize Roho. Usihisi kama unapaswa kutumia mawazo katika muhtasari huu. Unawajua watoto unaowafundisha; muombe Baba wa Mbinguni akuongoze kwenye njia bora za kuwasaidia kujifunza kanuni za injili na kujenga imani yao.

Chapisha