Mafundisho na Maagano 2021
Februari 1–7. Mafundisho na Maagano 10–11: “Kwamba Uweze Kutoka Mshindi”


“Februari 1–7. Mafundisho na Maagano 10–11: ‘Kwamba Uweze Kutoka Mshindi”,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)

“Februari 1–7. Mafundisho na Maagano 10–11,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2021

Muswada wa Kitabu cha Mormoni

Nakala ya muswada halisi wa Kitabu cha Mormoni.

Februari 1–7

Mafundisho na Maagano 10–11

“Kwamba Uweze Kutoka Mshindi”

Kwa sala soma Mafundisho na Maagano 10–11, ukitafakari jinsi unavyoweza kuwasaidia watoto kuelewa kweli katika sehemu hizi. Mawazo katika muhtasari huu—yote kwa ajili ya watoto wadogo na wakubwa—yanaweza kusaidia.

Andika Misukumo Yako

ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Waombe watoto kushiriki kile wanachokumbuka kutoka kwenye somo lililopita kuhusu Martin Harris na kurasa zilizopotea za tafsiri ya Kitabu cha Mormoni. Shiriki maelezo yoyote ambayo hawayakumbuki. Unaweza kutaka kurejelea “Sura ya 4: Martin Harris na Kurasa Zilizopotea” (Hadithi za Mafundisho na Maagano, 18–21).

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Mafundisho na Maagano 10:5.

Ninapoomba daima, Baba wa Mbinguni atanibariki.

Wakati mwingine watoto hudhani wanaweza kuomba tu kwa muda fulani na mahala fulani, na ikiwa tu wamepiga magoti au kufumba macho yao. Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia kujifunza jinsi ya “kuomba daima”?

Shughuli za Yakini

  • Onesha picha ya mambo tunayofanya mara nyingi, kama vile kula, kulala, au kucheza. Ni kwa jinsi gani mambo haya hutusaidia? Onesha picha ya mtoto akiomba wakati ukiwasomea watoto kutoka Mafundisho na Maagano 10:5 maneno “omba daima.” Waombe watoto warudie maneno haya mara kadhaa. Ni kwa jinsi gani kuomba daima kunatusaidia?

  • Tumia ukurasa wa shughuli ya wiki hii kuwasaidia watoto kufikiria juu ya sehemu nyingi na mara nyingi ambazo tunaweza kuomba.

  • Waalike watoto kuchora picha zao wenyewe au familia zao zikiomba katika nyakati tofauti na sehemu tofauti, kama vile kanisani, kabla ya kwenda shule, au wakati wa kulala. Elezea kwamba kuomba daima kunaweza kumaanisha kuomba mara nyingi katika siku. Ni kwa jinsi gani tunaweza kuomba hata wakati tunapokuwa kati ya watu, kama vile shuleni au tunapokuwa na rafiki zetu?

    wavulana wakicheza

    Bwana atatusaidia wakati tunapoomba.

Mafundisho na Maagano 11:12–13

Roho Mtakatifu huniongoza kutenda mema.

Hata katika umri mdogo, watoto wanaweza kuanza kutambua wakati Roho anapozungumza nao.

Shughuli za Yakini

  • Ficha balbu ya mwanga au tochi na picha ya uso wa furaha mahala fulani katika chumba. Waombe watoto kutafuta vitu hivi. Soma Mafundisho na Maagano 11:13, na wasaidie watoto kutambua maneno ambayo yanahusiana na vitu walivyopata. Ni nini maneno haya hutufundisha kuhusu jinsi Roho Mtakatifu anavyotusaidia?

  • Wape watoto hali kadhaa ambazo kwazo wangehitajika kufanya uchaguzi kati ya jema na baya—kama vile uchaguzi wa kusema ukweli au kusema uongo, au uchaguzi wa kuwa mkarimu au kuwa mkatili. Ni kwa jinsi gani tunaweza kujua uchaguzi upi ni sahihi? Someni pamoja Mafundisho na Maagano11:12, na shuhudia kwamba Roho Mtakatifu atatusaidia kufanya uchaguzi sahihi ikiwa tutamsikiliza Yeye.

  • Imbeni wimbo kuhusu mwongozo wa Roho Mtakatifu, kama vile “Listen, Listen” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto,107). Waulize watoto wimbo unawafundisha nini kuhusu jinsi Roho Mtakatifu anavyotusaidia.

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Mafundisho na Maagano 10:5.

Ninapoomba daima, ninaweza kushinda majaribu ya shetani.

Unawezaje kuwasaidia watoto kuelewa kwamba maombi thabiti huwapa nguvu za kushinda majaribu.

Shughuli za Yakini

  • Andika maneno au virai kutoka Mafundisho na Maagano 10:5 kwenye vipande vya karatasi, na waombe watoto waviweke katika mpangilio sahihi. Wahimize kuangalia mstari ikiwa wanahitaji msaada. Kulingana na mstari huu, ni baraka zipi huja wakati tunapoomba daima? Ni kwa jinsi gani kukumbuka kuomba katika siku yetu hutusaidia, hasa wakati tunapojaribiwa kufanya jambo baya?

  • Waalike watoto kutengeneza orodha ya baadhi ya nyakati ambapo tunaweza kuomba na mahala ambapo tunaweza kuomba. Kwa mawazo ya ziada, wahimize kuangalia katika Alma 34:17–27.

  • Wasaidie watoto kutengeneza alama ndogo au picha ambayo itawakumbusha kuomba daima. Waalike kutundika alama yao katika nyumba zao mahala ambapo wataziona mara kwa mara.

Mafundisho na Maagano 11:12–13

Roho Mtakatifu huniongoza kutenda mema.

Vijana mara nyingi hujiuliza vile mwongozo wa Roho Mtakatifu unavyokuwa. Unaweza kutumia Mafundisho na Maagano 11 kuwafundisha watoto jinsi ya kutambua “Roho yule ambaye huongoza kufanya mema” (mstari wa 12).

Shughuli za Yakini

  • Wasaidie watoto kutengeneza orodha ya watu wanaowaendea wakati wanapohitaji msaada au wanapokuwa na swali. Kwa nini tunaamini kwamba watu hawa watatusaidia? Waalike watoto wasome Mafundisho na Maagano 11:12 na kutafuta kile Hyrum Smith alichoambiwa kuamini. Nini tunajifunza kutokana na mstari huu kuhusu kwa nini tunapaswa kuamini katika mwongozo wa Roho Mtakatifu?

  • Waulize watoto kile ambacho wangemwambia rafiki ambaye aliuliza vile inavyokuwa wakati Roho Mtakatifu anapozungumza nao. Waalike watoto kusoma Mafundisho na Maagano 11:12–13 ili kupata majibu yanayowezekana.

  • Shiriki pamoja na watoto baadhi ya uzoefu ulio nao wa Roho Mtakatifu kukuongoza kufanya mambo mema. Waalike watoto kutafakari wakati walipoweza kuwa walipata uzoefu kama huu na kisha shiriki uzoefu wao ikiwa wanahisi vizuri kufanya hivyo. Shuhudia kwamba Baba wa Mbinguni anataka kutuogoza kupitia Roho Mtakatifu. Wahimize watoto kugundua katika kipindi cha wiki ijayo wakati wanapokuwa na hisia kama zile zilizoelezewa katika Mafundisho na Maagano 11:12–13.

Mafundisho na Maagano 11:21,, 26.

Ninahitaji kujua injili ili niweze kuwasaidia wengine kupata ukweli.

Watoto unaowafundisha watakuwa na fursa nyingi za kushiriki injili. Mistari hii inaweza kuwafundisha jinsi ya kujiandaa kwa fursa hizi.

Shughuli za Yakini

  • Waalike watoto kuigiza jinsi ambavyo wangezungumza kuhusu injili na mtu ambaye hajawahi kuisikia kabla. Kwa mfano, ni kwa jinsi gani wangejibu maswali kuhusu Kitabu cha Mormoni? Ni kwa jinsi gani wangeelezea Yesu Kristo ni nani? Soma pamoja na watoto Mafundisho na Maagano 11:21, 26. Ni nini Bwana alimwambia Hyrum Smith kwamba alihitaji kufanya ili aweze kufundisha injili? Inamaanisha nini “kupata” neno la Mungu, na ni kwa jinsi gani tunaweza kufanya hili? Ni kwa jinsi gani “tunatunza katika hazina” neno la Mungu katika mioyo yetu?

  • Waalike watoto kushiriki andiko ambalo wanalipenda na waelezee kwa nini wanalipenda. Waruhusu wazungumze kuhusu jinsi maandiko yanavyobariki maisha yao na kile wanachofanya kujifunza neno la Mungu nyumbani. Wahimize kuweka malengo ya kusoma neno la Mungu mara kwa mara.

  • Imbeni pamoja wimbo kuhusu kushiriki injili, kama vile “I Want to Be a Missionary Now” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto,168). Ni nini wimbo huu unafundisha kuhusu jinsi tunavyoweza kuwa wamisionari kila siku?

  • Shiriki jambo kutoka katika “Tumaini la Israeli” na Rais Russell M. Nelson na Dada Wendy W. Nelson (mkutano wa ibada wa vijana ulimwenguni kote, Juni 3, 2018, ChurchofJesusChrist.org)

ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Waalike watoto kuwa na mazungumzo na mwanafamilia kuhusu jambo walilojifunza kutoka Mafundisho na Maagano 10 au 11 leo. Kwa mfano, wangeweza kushiriki jinsi wanavyopanga kuomba daima.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Tafuta ufunuo kila siku. Unapojiandaa kufundisha, omba na tafakari maandiko kwa wiki yote. Utakuta kwamba Roho “ataiangaza akili yako” (Mafundisho na Maagano 11:13). Mawazo na misukumo kuhusu jinsi ya kufundisha inaweza kukujia muda wowote na mahala popote—pale unapoenda kazini, unapofanya shughuli za nyumbani, au kuzungumza na wengine.