“Februari 15–21. Mafundisho na Maagano 14–17: ‘Simama kama Shahidi,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)
“Februari 15–21. Mafundisho na Maagano 14–17,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2021
Februari 15–21
Mafundisho na Maagano 14–17
“Simama kama Shahidi”
Ni kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia watoto kusimama kama mashahidi wa injili? Shughuli katika muhtasari huu zinaweza kukupa mawazo.
Andika Misukumo Yako
Alika Kushiriki
Fikiria kuwaalika watoto wachache kushiriki jambo walilojifunza wiki hii, nyumbani au katika Msingi, ambalo wanaamini ni la kweli.
Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo
Ninaweza kumsaidia Bwana kufanya kazi Yake.
Fikiria ni kwa jinsi gani maneno ya Bwana kwa David Whitmer yanaweza kuwasaidia watoto kuelewa jinsi wanavyoweza kushiriki katika kazi ya Bwana.
Shughuli za Yakini
-
Kwa ufupi shiriki maelezo machache kuhusu familia ya Whitmer (ona Watakatifu, 1:68–71 au muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia). Kwa mfano, shiriki David Whitmer alikuwa nani na jinsi yeye na familia yake walivyomsaidia Joseph Smith pale alipokuwa akitafsiri Kitabu cha Mormoni.
-
Wasaidie watoto kuelewa mfanano kati ya kufanya kazi shambani na kushiriki katika “kazi kubwa na ya ajabu” ya Mungu (mstari wa 1). Kwa mfano, kuvuna mazao kunaweza kuwakilisha kuleta nafsi kwa Kristo. Ungeweza kuonesha picha ya mkulima, kuleta nguo za mkulima kwa ajili ya watoto kujaribu kuvaa, au kujadili kazi za kila siku ambazo wakulima hufanya. Elezea kwamba David Whitmer alikuwa mkulima aliyetaka kujua jinsi ambavyo angeweza kumsaidia Bwana. Wasomee watoto Mafundisho na Maagano 14:3–4, na uwasaidie kugundua kile Bwana alichomwambia David Whitmer kufanya. Ni kwa jinsi gani tunaweza kusaidia katika kazi ya Bwana?
-
Tumia zawadi kuwafundisha watoto kuhusu zawadi ya Mungu ya uzima wa milele. Kwa mfano, waoneshe watoto zawadi ikiwa na karatasi ndani inayosomeka, “Uzima wa Milele” (Mafundisho na Maagano 14:7). Muache mtoto afungue zawadi, na usome Mafundisho na Maagano 14:7 kwa sauti. Shiriki kwamba uzima wa milele humaanisha kuishi milele na Mungu na kuwa kama Yeye. Shiriki ushuhuda wako juu ya baraka za kutii amri na kupokea uzima wa milele.
Mafundisho na Maagano 15:6; 16:6
Ninaweza kuwasaidia wengine kuja karibu na Yesu Kristo.
John Whitmer na Peter Whitmer Mdogo walikuwa kaka zake na David Whitmer. Kama David, walitaka kujua ni kwa jinsi gani wangeweza kumsaidia Bwana. Bwana aliwaomba kusaidia “kuleta nafsi Kwake.”
Shughuli za Yakini
-
Waombe watoto kuelezea jambo ambalo ni muhimu au lenye thamani kwao (kama vile kikaragosi, kitabu, au mchezo). Soma Mafundisho na Maagano 15:6 au 16:6, na waombe watoto kuinua mikono yao pale wanaposikia kile Bwana alichosema ni cha “thamani kubwa.”
-
Pamoja na watoto, tengenezeni orodha ya jinsi wanavyoweza kumsaidia mtu kumfuata Yesu Kristo, kama vile kuwa rafiki kwa wengine, kushiriki maandiko na rafiki, au kuomba kwa ajili ya mtu mwenye uhitaji. Ili kuwapa watoto mawazo, ungeweza kuonesha baadhi ya picha husika kutoka kwenye majarida ya Kanisa au Kitabu cha Sanaa ya Injili. Au watoto wangeweza kuchora picha zao wenyewe. Waalike kujaribu jambo katika orodha yao katika kipindi cha wiki.
Ninaweza kuwa shahidi juu ya mambo ambayo Mungu amenifanyia.
David Whitmer alikuwa mmoja wa Mashahidi Watatu wa Kitabu cha Mormoni, na wanne kati ya kaka zake walikuwa kati ya Mashahidi Wanane. Kama vile David na kaka zake, kila mmoja wetu anaweza “kusimama kama shahidi” wa ukweli (Mafundisho na Maagano 14:8).
Shughuli za Yakini
-
Waambie watoto kuhusu Mashahidi Watatu na Wanane (ona “Sura ya 7: Mashahidi Wanaona Bamba za Dhahabu” [Hadithi za Mafundisho na Maagano, 31–33], au video inayohusiana kwenye ChurchofJesusChrist.org). Waalike watoto kuchora picha ya mashahidi wakiangalia mabamba.
-
Waalike watoto kupaka rangi ukurasa wa shughuli ya wiki hii, na kuutumia kusimulia tukio la Mashahidi Watatu.
-
Nyanyua nakala ya Kitabu cha Mormoni, na wasomee watoto mstari wa mwisho wa Mafundisho na Maagano 17:6: “Kama vile Bwana wenu na Mungu wenu aishivyo ni kweli.” Waambie watoto jinsi unavyojua Kitabu cha Mormoni ni cha kweli. Waalike watoto kuwa mashahidi wa Kitabu cha Mormoni kwa kukisoma na kuomba ili kujua ikiwa ni cha kweli na kisha kushiriki ushuhuda wao kwa wengine.
Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa
Ninaweza kumsaidia Bwana kufanya kazi Yake.
Pale unapojadili mafunuo kwa kaka za Whitmer, unaweza kushiriki baadhi ya njia ambazo Bwana hutualika kila mmoja wetu kumsaidia Yeye katika kazi Yake.
Shughuli za Yakini
-
Shiriki hadithi kuhusu David Whitmer na familia yake ambayo unahisi itakuwa yenye ushawishi kwa watoto (ona Watakatifu, 1:68–71). Ni kwa jinsi gani Bwana aliwatumia akina Whitmer kusaidia kujenga ufalme Wake?
-
Kwenye vipande vya karatasi, andika maswali rahisi na marejeleo ya maandiko yanayohusiana kutoka Mafundisho na Maagano 14–16. Kwa mfano: Neno la Mungu ni sawa na nini? (14:2). Kipawa kikuu cha Mungu ni kipi? (14:7). Ni nini ambacho Bwana anasema ni cha thamani kubwa? (15:6; 16:6). Mualike kila mtoto kuchagua swali na kutafuta majibu katika mistari.
-
Andika vichwa viwili vya habari ubaoni: Kazi ya Shamba na Kazi ya Bwana. Wasaidie watoto kupekua Mafundisho na Maagano 14:3–4 kwa ajili ya virai ambavyo vinahusiana na kazi ya shamba, na viandike chini ya kichwa cha habari cha kwanza. Ni nini virai hivi hutufundisha kuhusu kazi ya Mungu? Andika majibu ya watoto chini ya kichwa cha habari cha pili. Ni kwa jinsi gani tunaweza kusaidia katika kazi ya Bwana?
Ninaweza kuwa shahidi juu ya mambo ambayo Mungu amenifanyia.
Katika Mafundisho na Maagano 17, Bwana alimwambia Oliver Cowdery, David Whitmer, na Martin Harris kwamba wangekuwa Mashahidi Watatu wa Kitabu cha Mormoni. Wasaidie watoto kujifunza jinsi wanavyoweza pia kuwa shahidi wa ukweli.
-
Waalike watoto waje wakiwa wamejitayarisha kushiriki tukio la Mashahidi Watatu (ona “Sura ya 7: Mashahidi Wanaangalia Bamba za Dhahabu” [Mafundisho na Maagano, 31–33], au video inayohusiana ChurchofJesusChrist.org). Nini tunaweza kujifunza kutokana na tukio hili kuhusu jinsi ya kuwa mashahidi jasiri? Ungeweza pia kuonesha chaguo kutoka kwenye video “A Day for the Eternities” (ChurchofJesusChrist.org; kipengele kuhusu Mashahidi Watatu kinaanza takribani 15:00).
-
Someni pamoja ahadi ya Bwana katika Mafundisho na Maagano 17:1–3, na wasaidie watoto kutafuta utimizwaji wake katika “Ushuhuda wa Mashahidi Watatu” katika Kitabu cha Mormoni.
-
Someni pamoja Mafundisho na Maagano 17:3–5 ili kupata kile Oliver Cowdery, Martin Harris, na David Whitmer walichoombwa kufanya baada ya kuona mabamba ya dhahabu. Ni nini baadhi ya kweli tunaweza kuzishuhudia? Simulia kuhusu jinsi ambavyo umeshiriki ushuhuda wako pamoja na wengine, na waalike watoto kushiriki uzoefu wowote waliowahi kuwa nao.
Himiza Kujifunza Nyumbani
Waalike watoto kusimama kama shahidi wa jambo walilojifunza darasani leo. Waombe kushiriki jinsi walivyofanya hili katika darasa la wiki ijayo.