“Februari 8–14. Mafundisho na Maagano 12–13: Joseph Smith—Historia ya 1:66–75: ‘Juu Yenu Ninyi Watumishi Wenzangu,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Mafundisho na Maagano 2021 (2020)
“Februari 8–14. Mafundisho na Maagano 12–13: Joseph Smith—Historia ya 1:66–75,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2021
Februari 8–14
Mafundisho na Maagano 12–13; Joseph Smith—Historia ya 1:66–75
“Juu Yenu Ninyi Watumishi Wenzangu”
Joseph Smith na Oliver Cowdery walipokea elimu ya ziada waliposali kuhusu kweli walizojifunza katika maandiko (ona Joseph Smith—Historia ya 1:68). Je! unaweza kufuata mifano yao?
Andika Misukumo Yako
Watu wengi ulimwenguni kote labda kamwe hawajasikia sehemu inayoitwa Harmony, Pennsylvania. Lakini Bwana mara nyingi huchagua mahali pasipojulikana kwa ajili ya matukio mengi muhimu katika ufalme Wake. Katika eneo la msitu karibu na Harmony mnamo mei 15, 1829, Yohana Mbatizaji alitokea kama kiumbe aliyefufuka kwa Joseph Smith na Oliver Cowdery. Aliweka mikono yake juu ya vichwa vyao na kuwatunukia Ukuhani wa Haruni juu yao, akiwaita “watumishi wenzangu” (Mafundisho na Maagano 13:1).
Kufikiriwa kama mtumishi mwenza wa Yohana Mbatizaji, aliyembatiza Mwokozi na kutayarisha njia kwa ajili ujio Wake (ona Mathayo 3:1–6, 13–17)), lazima ilikuwa ya kunyenyekeza, labda hata furaha iliyopitiliza kwa vijana hawa wawili wenye umri wa miaka ya ishirini. Wakati ule, Joseph na Oliver kwa kiasi walikuwa hawajulikani, sawa sawa kama Harmony ilivyokuwa. Lakini huduma katika kazi ya Mungu kila siku imekuwa kuhusu jinsi tunavyohudumia, sio kuhusu nani anaangalia. Licha ya udogo au kutoonekana kwa mchango wako kunavyoweza kuwa wakati mwingine, wewe pia ni mtumishi mwenza katika kazi kuu ya Bwana.
Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko Kibinafsi
Bwana ananitaka mimi kusaidia kuanzisha kusudi la Sayuni.
Joseph Knight Mkubwa na mke wake, Polly, walikutana na Joseph Smith wakati, akiwa na umri wa miaka 20, alianza kufanya kazi kwenye shamba lao huko Colesville, New York. Joseph Knight anamwelezea kama mfanyakazi bora ambaye aliwahi kuwa naye. Aliamini ushuhuda wa Joseph Smith kuhusu mabamba ya dhahabu na alimchukua Polly kumtembelea Joseph Smith alipokuwa akitafsiri Kitabu cha Mormoni nyumbani kwake huko Harmony, Pennsylvania. Polly mara moja aliamini. Kwa maisha yao yote, Joseph na Polly walibaki waaminifu kwenye injili ya urejesho. Zaidi ya wanafamilia 60 wa familia ya Knight walijiunga na walisaidia kuanzisha Kanisa huko New York, Ohio, Missouri, Nauvoo, na hatimaye Jiji la Salt Lake.
Joseph Night alitaka kujua jinsi ambavyo angeweza kusaidia katika kazi ya Bwana. Jibu la Bwana (sasa Mafundisho na Maagano 12) linatumika kwa “wale wote walio na hamu ya kuanzisha na kuendeleza kazi hii” (mstari wa 7)—ikiwa ni pamoja na wewe. Ina maana gani kwako “kuanzisha na kustawisha kusudi la Sayuni”? (mstari wa 6). Ni kwa jinsi gani kanuni na sifa katika mstari 7–9 zinakusaidia wewe kufanya hivi?
Ona pia “Familia za Knight na Whitmer,” Funuo katika Muktadha, 20–24.
Ukuhani wa Haruni ulirejeshwa na Yohana Mbatizaji.
Katika sentensi moja tu, Yohana Mbatizaji alifunua kweli nyingi kuhusu Ukuhani wa Haruni. Fikiria kuorodhesha kila kitu unachojifunza kutoka sehemu hii (ikijumuisha kutoka kichwa cha habari cha sehemu). Unaweza kuona inasaidia kujifunza baadhi ya virai unavyovipata. Hapa kuna baadhi ya mifano kukuwezesha kuanza:
-
“Funguo za huduma ya malaika”: 2 Nefi 32:2–3; Moroni 7:29–32; Jeffrey R. Holland, “Huduma ya Malaika,” Ensign au Liahona, Nov. 2008, 29–31; Mwongozo kwenye Maandiko, “Malaika,” scriptures.ChurchofJesusChrist.org
-
“Funguo … za injili ya toba”: 3 Nefi 27:16–22; Mafundisho na Maagano 84:26–27; Dale G. Runlund, “Ukuhani na Nguvu ya Upatanisho ya Mwokozi,” Ensign au Liahona, Nov. 2017, 64–67
-
“Wana wa Lawi”: Hesabu 3:5–13; Mafundisho na Maagano 84:31–34; Mwongozo wa Maandiko, “Ukuhani wa Haruni,” “Lawi,” scriptures.ChurchofJesusChrist.org
Ni baraka gani umezipokea kupitia ibada za Ukuhani wa Haruni?
Joseph Smith—Historia ya 1:66–75
Ibada zinaniwezesha kufikia nguvu ya Mungu.
Dada Carole M. Stephens, aliyekuwa mshauri wa Urais Mkuu wa Muungano wa Usaidizi wa Akina Mama, alifundisha: “Ibada za Ukuhani na maagano vinaleta upatikanaji kwa ukamilifu wa baraka tulizoahidiwa na Mungu, ambazo zimefanywa ziwezekane kwa upatanisho wa Mwokozi. Zinawalinda wana na mabinti wa Mungu kwa nguvu, nguvu ya Mungu, na hutupatia fursa ya kupokea uzima wa milele” (“Je, Tunajua Nini Tulicho Nacho?” Ensign au Liahona, Nov. 2013, 12).
Unaposoma Joseph Smith—Historia ya 1:66–75, pamoja na muhtasari mwishoni mwa mstari wa 71, fikiria nini kiliwatia msukumo Joseph na Oliver kuuliza kuhusu ubatizo, na gundua baraka ambazo ziliwajia baada ya kushiriki katika ibada za ukuhani. Fikiria kusoma maingizo ya shajara ambayo umeweza kuyaandika baada ya kupokea ibada au kurekodi mawazo yako ya matukio hayo. Ni baraka gani ulizozipokea kupitia ibada za ukuhani?
Ona pia Mafundisho na Maagano 84:20–22; Watakatifu, 1:65–68.
Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko Kifamilia na Jioni ya Familia Nyumbani
-
Mafundisho na Maagano 12:8.Kwa nini sifa zilizoorodheshwa katika kifungu hiki ni muhimu wakati tunapofanya kazi ya Bwana?
-
Mafundisho na Maagano 13.Nini kinaweza kujenga imani ya familia yako katika urejesho wa Ukuhani wa Haruni? Video ya “Urejesho wa Ukuhani wa Haruni” (ChurchofJesusChrist.org) au kazi ya sanaa ambayo inaambatana na muhtasari huu ingeweza kusaidia familia yako kupata taswira ya urejesho wa Ukuhani wa Haruni. Je, wangefurahia kuchora picha ya tukio, kulingana na kile wanachosoma katika Joseph Smith—Historia ya 1:68–74? Wangeweza pia kushiriki shuhuda zao kuhusu uwezo wa ukuhani katika maisha yao.
Ona pia “Sehemu ya Urejesho wa Ukuhani” kwenye history.ChurchofJesusChrist.org.
-
Joseph Smith—Historia ya 1:68.Ni kwa jinsi gani tunaweza kufuata mfano wa Joseph Smith na Oliver Cowdery kutafuta majibu kwa maswali yetu? Labda mnaposoma pamoja, mngeweza kuifanya tabia ya mara kwa mara kutulia na kuuliza kama yeyote ana swali kuhusu kile wanachosoma.
-
Joseph Smith—Historia ya 1:71, muhtasari.Ni nini kinawavutia wanafamilia yako kuhusu maneno ya Oliver Cowdery? Ni zipi baadhi ya “siku ambazo kamwe hazitasahaulika” za familia yako?
-
Joseph Smith—Historia ya 1:73–74Ni athari gani Roho Mtakatifu alikuwa nazo kwa Joseph na Oliver? Ni lini Roho Mtakatifu amesaidia familia yako kuelewa maandiko na kufurahi katika Bwana?
Kwa mawazo zaidi kwa ajili ya kuwafundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Msingi.
Wimbo uliopendekezwa: “The Priesthood Is Restored,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto,89.