Scripture Stories
Sura ya 51: Yesu Anateseka katika Bustani ya Gethsemane


Sura ya 51

Yesu Anateseka katika Bustani ya Gethsemane

Picha
Yesu na Mitume katika Bustani ya Gethsemane

Yesu na Mitume walienda kwenye Bustani ya Gethsemane. Yuda hakwenda pamoja nao. Alienda kuwaambia viongozi wa Kiyahudi mahali Yesu alipokuwa.

Picha
Yesu akizungumza na Mitume

Yesu aliwaomba Petro, Yakobo na Yohana kwenda pamoja Naye katika bustani. Aliwasihi wamngoje wakati alipokwenda kuomba.

Picha
Yesu akiomba

Yesu alijua alihitaji kuteseka kwa ajili ya dhambi za watu wote. Hakutaka kuteseka, lakini alichagua kumtii Baba wa Mbinguni.

Picha
Yesu akiwaamsha Mitume

Petro, Yakobo, na Yohana walilala wakati Yesu akiomba. Yesu alikuja na kuwakuta wamelala. Aliwaambia wawe macho.

Picha
Yesu akiwaangalia Mitume waliolala

Alienda kuomba tena. Petro, Yakobo na Yohana walitaka kubaki macho, lakini walikuwa wamechoka sana. Walilala tena. Yesu aliwakuta wamelala tena. Alienda na kuomba kwa mara ya tatu.

Picha
malaika akimfikia Yesu

Yesu alipokuwa akisali, Alianza kutetemeka kwa sababu ya uchungu. Malaika alikuja kumpa nguvu. Aliteseka sana kiasi kwamba alitokwa na jasho la matone ya damu. Alikuwa akiteseka kwa ajili ya dhambi zetu ili kwamba tuweze kusamehewa tukitubu.

Picha
kundi la watu wenye fujo likimjia Yesu na Mitume

Yesu aliwaamsha Petro, Yakobo na Yohana. Aliwaambia kwamba angesalitiwa na kuuwawa. Yesu alisema kwamba watu waovu walikuwa wanakuja kumchukua.

Chapisha