Scripture Stories
Sura ya 16: Mwana wa Kiongozi


Sura ya 16

Mwana wa Kiongozi

Picha
mtu pembeni mwa kitanda cha mwanawe

Kiongozi wa Wayahudi alikuwa na mwana aliyekuwa mgonjwa sana. Kila mtu alifikiria kwamba mwana wake angekufa punde.

Picha
watu wakipanda farasi

Mtu huyo alimwacha mwanawe nyumbani na kusafiri maili nyingi kwenda mji wa Kana. Hapo alimpata Yesu.

Picha
mtu akizungumza na Yesu

Mtu huyo alimwomba Mwokozi aje amponye mwanawe. Yesu alimwambia kwamba mwanawe angeponywa. Mtu huyo alimwamini Yesu, na akaanza safari kuelekea nyumbani.

Picha
watumishi wakimkimbilia mtu

Watumishi wake walikuja kukutana naye. Walimwambia kwamba mwanawe alikuwa anasikia nafuu na angeishi. Aliwauliza ni wakati gani mwanawe alianza kusikia nafuu. Walimwambia. Ilikuwa ni wakati ule ule Yesu alipokuwa amesema kwamba huyo mwana angeponywa.

Picha
mtu anamtabasamia mwanawe

Mtu huyo alijua kwamba Yesu Kristo alikuwa amemponya mwanawe. Yeye na familia yake yote waliamini katika Mwokozi.

Chapisha