Scripture Stories
Sura ya 40: Mchungaji Mwema


Sura ya 40

Mchungaji Mwema

Picha
Yesu amemshikilia mwana kondoo

Mchungaji kondoo huwatunza kondoo. Huwasaidia kupata chakula na maji. Hawaachi waumie ama wapotee. Anawajua na kuwapenda na angeweza kutoa maisha yake ili kuwaokoa.

Picha
Yesu na wanafunzi

Yesu Kristo alijiita Mchungaji Mwema. Yeye ni mchungaji wetu. Sisi ni kondoo Wake. Anatupenda. Anatusaidia kujifunza ukweli. Anatufundisha jinsi ya kuishi ili tuweze kurudi kwa Baba wa Mbinguni. Alitoa maisha Yake kwa ajili Yetu.

Picha
Yesu akiwafundisha wanafunzi

Yesu aliwaambia watu kule Yerusalemu kwamba Yeye alikuwa na kondoo wengine. Alisema angewatembelea hawa kondoo wengine. Watu hawakuelewa.

Picha
Yesu akiwafundisha wanafunzi

Baada Yesu kufufuka, aliwatembelea kondoo Wake wengine huko Amerika. Kitabu cha Mormoni kinasimulia kuhusu matembezi Yake huko. Yesu alikaa siku nyingi, akiponya wagonjwa na kuwabariki watu. Aliwapa wao ukuhani na kuanzisha Kanisa Lake. Yesu alifundisha mambo yale yale kwa watu hawa ambayo alikuwa amewafundisha watu kule Yerusalemu.

Chapisha