Scripture Stories
Sura ya 3: Yohana Mbatizaji Azaliwa


Sura ya 3

Yohana Mbatizaji Azaliwa

Picha
malaika akizungumza na Mariamu

Malaika Gabrieli alimwambia Mariamu kwamba Elisabeti pia alikuwa akitarajia mtoto wa kiume. Mariamu na Elisabeti walikuwa ndugu.

Picha
Mariamu na Elisabeti

Mariamu alikwenda kumtembelea Elisabeti. Roho Mtakatifu alimwambia Elisabeti kwamba Mariamu angekuwa mama wa Yesu Kristo. Mariamu na Elisabeti walimshukuru Mungu kwa kuwabariki. Mariamu aliishi na Elisabeti kwa takriban miezi mitatu. Kisha Mariamu akaenda nyumbani Nazareti.

Picha
Elisabeti na familia pamoja na mtoto

Mwana wa Elisabeti alizaliwa. Marafiki zake na familia walifurahi. Walifikiria kwamba mtoto alifaa kuwa na jina sawa na la baba yake, Zakaria. Lakini Elisabeti alisema kwamba jina lake lilipaswa kuwa Yohana. Kila mtu alishangaa.

Picha
Zakaria akiandika

Watu walimuuliza Zakaria jina la mtoto lilipaswa kuwa lipi. Zakaria bado alikuwa hawezi kuongea, hivyo aliandika, “Jina lake ni Yohana.”

Picha
Zakaria akitabasamu

Kisha Zakaria aliweza kuzungumza tena. Alijazwa na Roho Mtakatifu. Aliwaambia watu kwamba Yesu Kristo angezaliwa karibuni na kwamba Yohana angewatayarisha watu kwa ajili Yake.

Picha
mtoto ndani ya kitanda cha mtoto

Yohana alikua na akawa nabii mashuhuri. Alifundisha watu kuhusu Yesu Kristo.

Chapisha