Sura ya 57 Watu Waovu Wanamwua Stefano Viongozi wengi wa Kiyahudi walifikiri kwamba miujiza ingekoma Yesu alipokufa. Lakini, Mitume pia walifanya miujiza. Watu wengi waliamini katika Yesu Kristo na kujiunga na Kanisa. Matendo ya Mitume 4:1–4, 13–16; 5:14 Hii iliwakasirisha viongozi wengi wa Kiyahudi. Waliwaweka Petro na Yohana gerezani. Mfalme Herode Agripa alifanya Mtume Yakobo auwawe. Matendo ya Mitume 4:3–21; 12:1–2 Mitume waliwaita watu saba wasaidie kuongoza Kanisa. Mmoja alikuwa mtu mwadilifu aliyeitwa Stefano. Alifundisha injili kwa watu wengi. Baadhi ya watu walidanganya na kusema kwamba Stefano alizungumza kinyume cha sheria ya Wayahudi. Walimpeleka kuhukumiwa na viongozi wa Wayahudi. Matendo ya Mitume 6:3–12 Stefano aliwaambia viongozi kwamba walikuwa waovu. Alisema kwamba walikuwa wamemwua Yesu Kristo, Mwana wa Mungu. Matendo ya Mitume 7:51–54 Kisha Stefano alitazama juu mbinguni na kuwaona Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo. Alipowaambia viongozi kile alichoona, walikasirika sana. Matendo ya Mitume 7:55–56 Walimchukua Stefano nje ya mji ili kumwua kwa kumpiga na mawe. Waliweka nguo zao miguuni mwa kijana mmoja aliyeitwa Sauli. Stefano alipokuwa anakufa, alimwomba Mungu aichukue roho yake mbinguni. Pia alimwomba Mungu awasamehe wale ambao walikuwa wakimwua. Kisha alikufa. Matendo ya Mitume 7:58–60