Hadithi za Maandiko
Sura ya 52: Mashitaka ya Yesu


Sura ya 52

Mashitaka ya Yesu

kundi la watu wenye fujo wakiwa na tochi

Viongozi wa Wayahudi walituma watu wenye mapanga na fimbo kwenye Bustani ya Gethsemane.

Yuda akiwa na kundi la watu wenye fujo

Yuda Iskariote alikuwa pamoja nao. Makuhani wakuu walikuwa wamemlipa Yuda ili kuwaonyesha watu wale mahali Yesu alipokuwa.

Yuda amesimama kando ya Yesu

Yuda aliwaonyesha watu wale Yesu alikuwa yupi kwa kumbusu. Watu wale walimchukua Yesu. Walimkejeli na kumpiga. Kisha walimpeleka Yesu kwa kuhani mkuu, Kayafa.

watu wakimwuliza Yesu maswali

Viongozi wa Kiyahudi walimwuliza Yesu maswali. Walisema kwamba alikuwa amevunja sheria kwa kusema kwamba Yeye alikuwa Mwana wa Mungu. Yesu aliwaambia kwamba Yeye alikuwa Mwana wa Mungu. Walisema Yesu alikuwa na hatia na alipaswa afe.

Yesu amesimama mbele ya Pilato

Viongozi wa Kiyahudi hawakuwa na mamlaka ya kumwua Yesu. Walimpeleka kwa Pontio Pilato, ambaye angeweza kumhukumu Yesu kifo. Viongozi wa Kiyahudi walimwambia Pilato kwamba Yesu alikuwa amewafundisha watu kutotii sheria ya Kirumi.

kundi la watu wenye fujo wakiwa na hasira

Pilato hakufikiri Yesu alikuwa amefanya chochote kibaya. Pilato alitaka kumwachia Yesu. Umati ulitaka Yesu asulubiwe.

Pilato akizungumza na Yesu

Pilato bado alitaka kumwachia Yesu. Lakini makuhani na watu waliendelea kupiga kelele kwamba walitaka Yesu asulubiwe.

Pilato akiosha mikono yake

Pilato aliosha mikono yake. Alisema kwamba hakuhusika na kifo cha Yesu. Watu walisema kwamba wangewajibika kwa ajili ya kifo Chake. Pilato aliwaambia askari wake wamsulubishe Yesu.