Hadithi za Maandiko
Utangulizi: Mpango wa Baba Yetu wa Mbinguni


Utangulizi

Mpango wa Baba Yetu wa Mbinguni

watoto wakiwa mbinguni na Baba wa Mbinguni

Tuliishi mbinguni na Baba wa Mbinguni kabla ya kuja duniani. Sisi ni watoto Wake wa kiroho na tulikuwa na miili ya kiroho. Tulimpenda, Naye alitupenda.

Mafundisho ya Nabii Joseph Smith, 354

watu mbinguni wakiwa na Baba wa Mbinguni

Baba wa Mbinguni alitufundisha kuhusu mpango Wake kwa ajili yetu. Unaitwa mpango wa wokovu. Tukiufuata mpango Wake, tunaweza kuwa kama Baba wa Mbinguni. Mpango ulikuwa kwetu sisi kuja duniani na kuwa na miili ya nyama na damu. Tungejaribiwa ili kuona kama tungechagua kutii amri za Mungu.

Baba wa Mbinguni akizungumza na Yesu pamoja na Shetani

Mpango wa wokovu unatoa njia kwetu sisi kuishi na Baba wa Mbinguni tena. Tungehitajika kutii amri. Lakini pia tungehitaji usaidizi. Tungehitaji dhambi zetu kuondolewa, na tungehitaji miili iliyofufuka. Kwa sababu hatuwezi kuziondoa dhambi zetu wenyewe au kufufua miili yetu wenyewe, tulihitaji Mwokozi kufanya hili kwa ajili yetu.

Baba wa Mbinguni akizungumza na Yesu

Baba wa Mbinguni alimchagua Yesu Kristo kuwa Mwokozi wetu. Yesu alimpenda Baba wa Mbinguni. Yesu pia alitupenda. Alikubali kuja duniani ili kutuonyesha jinsi ya kuwa wenye haki. Angetoa njia kwetu sote kuokolewa. Alikubali kuteseka kwa ajili ya dhambi zetu. Angekufa pia na kufufuka ili tuweze kufufuka vilevile.

Shetani

Shetani pia alitaka kuwa mwokozi wetu. Lakini hakumpenda Baba wa Mbinguni. Hukutupenda sisi. Alitaka kubadilisha mpango wa Baba wa Mbinguni ili kwamba aweze kuwa na nguvu na utukufu wa Baba wa Mbinguni.

Shetani na wafuasi wake wakiondoka mbinguni

Baadhi ya watoto wa kiroho wa Baba wa Mbinguni walichagua kumfuata Shetani. Hii ilimfanya Baba wa Mbinguni kuhuzunika sana. Alifanya Shetani na wafuasi wake waondoke mbinguni. Shetani ndiye ibilisi. Yeye na roho waliomfuata wanataka sisi tutende dhambi.

Yesu akiumba dunia

Baba wa Mbinguni alimwambia Yesu aumbe dunia kwa ajili yetu. Yesu alifanya hivyo. Aliumba jua, mwezi, na nyota. Aliweka mimea na wanyama duniani. Sasa tulikuwa na dunia ambapo tungekuja ambapo tungekuwa na miili ya nyama na damu.

nabii wa kale akiwafundisha watu

Watu wengi huja kuishi duniani. Baadhi yao huchagua kutii amri za Mungu; wengine hawatii. Manabii wa kale waliwafundisha watu kuhusu mpango wa Baba wa Mbinguni na kuhusu Yesu Kristo.

nabii akiandika kuhusu kuzaliwa kwa Yesu

Manabii walisema baba wa Yesu angekuwa Baba wa Mbinguni. Mama yake angekuwa mwanamke mwema kabisa aitwaye Mariamu. Angezaliwa Bethlehemu.

nabii akifundisha kuhusu Yesu

Manabii walisema kwamba watu wengi wasingeamini kwamba Yesu alikuwa Mwokozi. Angeonekana kama watu wengine na asingekuwa tajiri. Watu wengi wangemchukia.

nabii akifundisha kuhusu Yohana Mbatizaji

Manabii pia walisema kuhusu Yohana Mbatizaji. Angekuja kabla ya Yesu ili kuwaambia watu kumhusu Yeye. Yohana angembatiza Yesu.

nabii akifundisha kuhusu Yesu

Manabii walisema kwamba Yesu angekuwa mkarimu na angetenda miujiza mingi. Kabla ya Yeye kufa, Yesu angeteseka kwa ajili ya dhambi za watu wote ili wao wasiteseke ikiwa wangetubu.

nabii akifundisha kuhusu kifo cha Yesu

Manabii wengi walijua kwamba Yesu Kristo, Mwokozi wetu, angesulubiwa. Angepigiliwa misumari kwenye msalaba wa mbao na angetoa maisha Yake kwa ajili yetu.

nabii akifundisha kuhusu Ufufuo

Baada ya siku tatu, Angefufuka. Roho yake ingerudi tena ndani ya mwili Wake. Kwa sababu Yesu angekufa na kufufuka, sote tungefufuka pia.

watu katika Agano Jipya

Agano Jipya linaonyesha kwamba maneno ya manabii ni ya kweli. Ni hadithi ya Yesu Kristo na Mitume Wake. Waliishi katika Nchi Takatifu. Wengi wa watu walioishi huko walikuwa wakiitwa Wayahudi. Warumi walikuwa wameteka Nchi Takatifu, na waliwatawala Wayahudi.