Scripture Stories
Sura ya 1: Elisabeti na Zakaria


Sura ya 1

Elisabeti na Zakaria

Picha
Zakaria na Elisabeti

Zakaria na mkewe, Elisabeti, walikuwa Wayahudi walioishi karibu na Yerusalemu. Walitii amri za Mungu. Kwa miaka mingi waliomba wapate mtoto. Walipokuwa wazee, bado hawakuwa na watoto.

Picha
malaika akizungumza na Zakaria

Zakaria alikuwa kuhani katika hekalu. Siku moja malaika aliyeitwa Gabrieli alimjia. Gabrieli alisema kwamba Mungu angejibu maombi ya Zakaria na Elisabeti. Wangepata mtoto. Gabrieli alisema walipaswa kumuita mtoto huyo Yohana.

Picha
malaika akizungumza na Zakaria

Gabrieli alisema kwamba Yohana angekuwa nabii wa Mungu mwenye haki. Angefundisha watu kuhusu Yesu Kristo.

Picha
malaika akizungumza na Zakaria

Zakaria hakumwamini malaika. Elisabeti alikuwa mzee sana kuwa na mtoto. Gabrieli alisema kwamba kwa sababu hakuamini kile ambacho Mungu alikuwa ameahidi, Zakaria asingeweza kuzungumza hadi Yohana atakapozaliwa.

Chapisha