Scripture Stories
Sura ya 46: Ujio wa Pili


Sura ya 46

Ujio wa Pili

Picha
Yesu akiwafundisha wanafunzi

Yesu alikuwa kwenye Mlima wa Mizeituni. Wanafunzi Wake walitaka kumuuliza Yesu maswali kadhaa. Waliuliza ni lini waovu wangeangamizwa. Walitaka pia kujua lini Yesu angekuja tena.

Picha
mtu akizungumza na umati

Yesu aliwaambia kwamba kabla ya Ujio Wake wa Pili, manabii wa uwongo wangedai kuwa wao ndio Kristo. Watu wengi wangewafuata. Lakini kama wafuasi Wake wangetii maneno Yake, wasingepumbazwa na manabii wa uongo. Wangeokolewa.

Picha
familia ikitembea kupitia kwenye magofu

Yesu pia alisema kwamba kabla hajaja tena, kutakuwa na vita vingi, njaa, magonjwa mabaya, na matetemeko ya ardhi. Watu wengi wataacha kuwasaidia wengine na kuwa waovu.

Picha
mtu akiondoka kutoka kwa wamisionari

Injili itahubiriwa duniani kote, lakini watu wengi hawatasikiliza.

Picha
nyota zikianguka

Jua litatiwa giza, mwezi hautatoa mwanga wake, na nyota zitaanguka kutoka mbinguni.

Picha
Yesu akiwatokea watu

Yesu Kristo atakapokuja tena, watu watamuona akija kutoka mawinguni kwa nguvu na utukufu mkuu. Atawatuma malaika Wake wawakusanye wenye haki pamoja.

Picha
familia ikiangalia picha ya Yesu

Tunaweza kujiandaa kwa ajili ya Ujio wa Pili kwa kufanya kile kilicho chema. Tutakapoona ishara ambazo Yesu aliahidi, tutajua kwamba ujio wa Mwokozi u karibu. Hakuna anayejua kwa uhakika lini Yesu atakuja tena. Kama tumejiandaa, tunaweza kuwa Naye.

Chapisha