Sura ya 5 Yesu Kristo Azaliwa Mfalme mkuu wa Rumi aliweka sheria kwamba kila mtu lazima alipe kodi. Yusufu na Mariamu waliishi Nazareti. Iliwabidi waende maili 65 (105km) hadi Bethlehemu kulipa kodi zao. Luka 2:1–5 Haikuwa rahisi kwa Mariamu kusafiri hadi Bethlehemu. Mtoto wake punde angezaliwa. Luka 2:4–5 Wakati Yusufu na Mariamu walipofika Bethlehemu, vyumba vyote vilikuwa vimejaa watu. Mariamu na Yusufu walilazimika kukaa ndani ya zizi. Zizi ni mahali ambapo wanyama huwekwa. Luka 2:6–7 Hapo mtoto alizaliwa. Mariamu alimfunika kwa nguo na kumlaza katika hori. Yusufu na Mariamu walimwita mtoto Yesu. Luka 2:7, 21 Usiku ambao Yesu alizaliwa, wachungaji walikuwa wakichunga kondoo wao makondeni karibu na Bethlehemu. Malaika aliwatokea. Wachungaji waliogopa. Luka 2:8–9 Malaika aliwaambia wasiogope. Alikuwa na habari njema: Mwokozi, Yesu Kristo, alikuwa amezaliwa Bethlehemu. Wangemkuta amelala katika hori. Luka 2:10–12 Wachungaji walienda Bethlehemu, ambako walimuona mtoto Yesu. Luka 2:15–16 Wachungaji walifurahi kumwona Mwokozi. Waliwaambia watu wengine kuhusu yote waliyokuwa wamesikia na kuona. Luka 2:17, 20