Scripture Stories
Sura ya 27: Akifanya Kazi ya Baba yake Duniani


Sura ya 27

Akifanya Kazi ya Baba yake Duniani

Picha
mtu amelala pembeni mwa bwawa

Kwenye siku‑kuu ya Wayahudi, Mwokozi alienda katika bwawa la Bethzatha huko Yerusalemu. Watu walikuwa na dhana kwamba wakati maji katika bwawa yakisogea, mtu wa kwanza kuingia majini angeponywa.

Picha
Yesu akizungumza na mtu

Yesu alimwona mtu karibu na bwawa ambaye alikuwa hajaweza kutembea kwa miaka 38. Ilikuwa ni Sabato. Yesu alimwuliza mtu yule kama alitaka kuponywa. Mtu huyo alisema hakuweza kuponywa kwa sababu kamwe asigeweza kuingia majini wa kwanza.

Picha
mtu akiondoka kutoka kwa Yesu

Yesu alimwambia mtu yule, “Simama, jitwike godoro lako, na uende.” Mtu yule aliponywa mara moja.

Picha
watu wakimkasirikia Yesu

Watu wengi wa Kiyahudi waliamini kwamba ilikuwa ni dhambi kufanya miujiza siku ya Sabato. Walitaka kumuua Yesu.

Picha
Yesu akiwafundisha watu

Yesu alijibu kwamba alikuwa akifanya siku ya Sabato kile tu ambacho Baba Yake angefanya.

Chapisha