Scripture Stories
Sura ya 23: Mtu Ambaye Hakuweza Kutembea


Sura ya 23

Mtu Ambaye Hakuweza Kutembea

Picha
Yesu akiwafundisha watu

Siku moja Yesu alikuwa akifundisha kikundi cha watu ndani ya nyumba.

Picha
watu wakiwa wamembeba mtu mwingine kitandani

Watu fulani walimbeba rafiki yao kitandani ili kumwona Yesu. Rafiki huyo hakuweza kutembea. Watu hao hawakuweza kumwingiza ndani ya nyumba kwa sababu ya watu wote waliokuwapo.

Picha
watu wakimshusha mtu aliye kitandani ndani ya nyumba

Watu walimchukua rafiki yao juu kwenye paa. Walitoa sehemu ya paa na kumshusha rafiki yao ndani ya nyumba.

Picha
Yesu akimponya mtu

Alipoiona imani kubwa ya watu hawa, Yesu alimwambia mtu mgonjwa kwamba dhambi zake zilikuwa zimesamehewa. Alimwambia achukue kitanda chake na aende nyumbani. Mtu huyo alisimama. Alikuwa ameponywa. Alichukua kitanda chake na kutembea kwenda nyumbani. Alikuwa na shukrani sana kwa Mungu.

Chapisha