Scripture Stories
Sura ya 62: Paulo Anamtii Roho Mtakatifu


Sura ya 62

Paulo Anamtii Roho Mtakatifu

Picha
Paulo akiomba

Roho Mtakatifu alimwambia Mtume Paulo aende Yerusalemu. Roho Mtakatifu alisema kwamba Paulo angewekwa gerezani. Paulo hakuogopa. Alimpenda Mwokozi na alifanya kile ambacho Roho Mtakatifu alikuwa amemwambia kufanya.

Picha
Paulo akizungumza na marafiki

Paulo aliwaaga rafiki zake. Alisema asingeonana nao tena. Aliwaambia waishi injili na kutii amri za Mungu. Paulo aliwaonya wasiwasikilize watu ambao wangejaribu kuwafundisha vitu ambavyo si vya kweli.

Picha
watu wakitazama mashua ikiondoka

Paulo aliwaambia wapendane na kutunzana. Alipiga magoti na kuomba pamoja nao. Kila mtu alilia. Walienda pamoja naye kwenye mashua na kumtazama Paulo akiondoka kwenda Yerusalemu.

Chapisha