Scripture Stories
Sura ya 42: Mvulana Tajiri


Sura ya 42

Mvulana Tajiri

Picha
Yesu akizungumza na mvulana

Siku moja mvulana tajiri alimjia Yesu na kumuuliza kile anachopaswa kufanya ili apate kwenda mbinguni.

Picha
Yesu akizungumza na mvulana

Mwokozi alimwambia awapende na kuwaheshimu baba na mama yake na asiue mtu yeyote au kudanganya au kuiba. Mvulana tajiri alisema alikuwa daima akitii amri.

Picha
Yesu akizungumza na mvulana

Yesu alimwambia mvulana yule kwamba alihitaji kufanya kitu kingine kimoja. Alihitaji kuuza kila kitu alichokuwanacho na kutoa pesa hizo kwa masikini. Kisha mvulana huyo alipaswa kumfuata Yeye.

Picha
mvulana akiondoka kutoka kwa Yesu

Mvulana tajiri hakutaka kutoa vyote alivyokuwanavyo. Alipenda vile vitu alivyokuwanavyo zaidi ya vile alivyompenda Mungu. Mvulana aliondoka akihuzunika.

Picha
Yesu akiwafundisha watu

Mwokozi aliwaambia wanafunzi Wake kwamba ni vigumu kwa wale wapendao mali kwenda mbinguni. Wanafunzi hawakuelewa. Waliuliza nani anaweza kuishi na Mungu. Yesu alisema kwamba watu wanaomtumainia Mungu na kumpenda zaidi ya kitu chochote kingine wanaweza kuishi Naye mbinguni.

Marko 10:23–30 (ona rejeo chini ya ukurasa 27a)

Chapisha