Scripture Stories
Sura ya 4: Yusufu na Malaika


Sura ya 4

Yusufu na Malaika

Picha
Yusufu na Mariamu

Yusufu alikuwa mtu mwema na mkarimu. Yeye na Mariamu walikuwa waoane. Alipofahamu kwamba Mariamu alikuwa mja mzito, hakujua nini cha kufanya. Kwa sababu mtoto hakuwa wake, alifikiria alipaswa kutomuoa.

Picha
malaika akimtokea Yusufu

Usiku mmoja malaika alimjia Yusufu katika ndoto na kumwambia kwamba mtoto wa Mariamu alikuwa Mwana wa Mungu. Malaika alimwambia Yusufu amwoe Mariamu na amwite mtoto wake Yesu. Yesu alikuwa awe Mwokozi wa ulimwengu.

Picha
Yusufu na Mariamu wakioana.

Yusufu alimtii malaika na kumwoa Mariamu.

Chapisha