Scripture Stories
Sura ya 6: Kuwasilishwa Hekaluni


Sura ya 6

Kuwasilishwa Hekaluni

Picha
Yusufu, Mariamu, na mtoto Yesu hekaluni

Yesu alipokuwa na umri wa wiki chache, wazazi Wake walimleta Yerusalemu ili kumwasilisha hekaluni.

Picha
Simeoni akiota ndoto juu ya Yesu Kristo

Simeoni, mtu mwenye haki aliyeishi Yerusalemu, alikuwa hekaluni. Roho Mtakatifu alimwambia angemwona Kristo kabla hajafa.

Picha
Simeoni akiwa amembeba mtoto Yesu

Simeoni alimwona mtoto Yesu hekaluni. Alimbeba mikononi mwake na kumsifu Mungu.

Picha
Simeoni akiwa amembeba mtoto Yesu

Simeoni alisema kwamba mtoto huyo angeleta wokovu kwa watu wote. Yusufu na Mariamu walistaajabu kwa yale aliyosema.

Picha
Ana akimuona mtoto Yesu

Mjane aliyeitwa Ana pia alimwona Yesu na alijua Yeye alikuwa nani. Alitoa shukrani na kuwaambia watu wengi kuhusu Yeye.

Chapisha