Scripture Stories
Sura ya 8: Mfalme Herode Mwovu


Sura ya 8

Mfalme Herode Mwovu

Picha
askari wakiua watoto

Mamajusi walikuwa wamemwambia Herode kwamba Yesu angekuwa mfalme. Herode alitaka kuwa mfalme pekee. Aliwaambia askari wake wawaue watoto wote katika Bethlehemu na viunga vyake.

Picha
malaika akimtokea Yusufu

Malaika alimwambia Yusufu awachukue Mariamu na Yesu hadi Misri, nchi iliyokuwa mbali na Bethlehemu. Herode asingemtafuta Yesu huko.

Picha
Yusufu, Mariamu, na Yesu wakisafiri

Yusufu alitii. Yeye na Mariamu na Yesu walikuwa Misri wakati askari wa Herode walipowaua watoto wote katika Bethlehemu na viunga vyake.

Picha
Yusufu, Mariamu, na Yesu wakisafiri

Baada ya Mfalme Herode kufa, malaika alimwambia Yusufu awapeleke Yesu na Mariamu nyumbani. Yusufu aliwapeleka Nazareti, ambapo Yesu alikuwa salama.

Chapisha