Sura ya 37 Wenye Ukoma Kumi Yesu alienda kwenye mji mdogo ambapo aliwaona wenye ukoma kumi. Wenye ukoma ni watu ambao ni wagonjwa. Ugonjwa wao huwasababishia kupata vidonda vibaya kote katika miili yao. Luka 17:12 Madaktari hawakuweza kuwasaidia wenye ukoma. Watu walikuwa na hofu kuwakaribia. Hawakutaka kuwa wagonjwa pia. Luka 17:12 Wenye ukoma walimsihi Yesu awaponye. Walijua angeweza kufanya vidonda vyao vipotee. Luka 17:13 Yesu aliwataka wawe wazima. Aliwaambia waende wajionyeshe kwa makuhani. Luka 17:14 Walipokuwa njiani kwenda kwa makuhani, wenye ukoma kumi waliponywa. Vidonda vyao vilikuwa vimetoweka. Luka 17:14 Mmoja wa wenye ukoma alijua kwamba Yesu alikuwa amewaponya. Alirudi kumshukuru Yesu. Yesu aliuliza walipokuwa wenye ukoma wengine tisa. Hawakuwa wamerudi. Yesu alimwambia mwenye ukoma aliyekuwa amemshukuru kwamba imani ya mwenye ukoma huyo ilikuwa imemponya. Luka 17:15–19