Hadithi za Maandiko
Sura ya 48: Talanta


Sura ya 48

Talanta

mtu akiwapa watumishi  watatu pesa

Yesu aliwaambia wanafunzi Wake hadithi ya mtu aliyewapa watumishi wake talanta kadhaa. Talanta ilikuwa ni kiasi kikubwa cha pesa.

watumishi watatu wameshikilia pesa

Mtu yule alimpa mtumishi mmoja talanta tano. Alimpa mtumishi mwingine talanta mbili. Alimpa mtumishi wa tatu talanta moja. Kisha mtu yule akaenda safari.

mtu akinunua dumu kutoka kwa mtu mwingine

Mtumishi aliyekuwa na talanta tano alifanya kazi kwa bidii. Alipata talanta tano zaidi. Sasa alikuwa na talanta kumi.

mtu akipima pesa

Mtumishi aliyekuwa na talanta mbili pia alifanya kazi kwa bidii. Alipata talanta mbili zaidi. Sasa alikuwa na talanta nne.

mtuakifukia pesa

Mtumishi aliyekuwa na talanta moja aliifukia ardhini. Alikuwa na hofu angeipoteza. Hakufanya kazi kupata talanta yoyote zaidi.

mtu akizungumza na watumishi watatu

Mtu yule aliporudi, aliwauliza watumishi kile walichokuwa wamefanya na talanta zake.

mtu akimpa pesa mtumishi

Mtumishi wa kwanza alimletea talanta kumi. Mtu yule alikuwa na furaha. Alimfanya mtumishi kuwa kiongozi juu ya mambo mengi na kumwambia awe na furaha.

mtu akimpa pesa mtumishi

Mtumishi wa pili alimletea mtu yule talanta nne. Hii pia ilimfanya mtu yule awe na furaha. Alimfanya mtumishi wa pili kuwa kiongozi juu ya mambo mengi na akamwambia awe na furaha.

mtumishi akimwonyesha mtu pesa

Mtumishi wa tatu alimrudishia mtu yule talanta ile aliyokuwa ameifukia. Mtu yule hakuwa na furaha. Alisema yule mtumishi alikuwa mvivu. Alipaswa kufanya kazi kwa bidii ili apate talanta zaidi.

mtu akimpa pesa mtumishi

Mtu yule aliichukua talanta kutoka kwa mtumishi wa tatu na kumpa mtumishi wa kwanza. Kisha akamfukuzia mbali mtumishi mvivu. Mtu yule katika hadithi ni kama Yesu. Sisi ni kama wale watumishi. Yesu atahukumu jinsi kila mmoja wetu anavyotumia karama ambazo tumepewa.