Scripture Stories
Sura ya 56: Petro Anamponya Mtu


Sura ya 56

Petro Anamponya Mtu

Picha
mtu akiomba pesa

Mtu aliyekuwa hawezi kutembea alibebwa na kupelekwa hekaluni kila siku. Aliketi kando ya milango wa hekalu na kuomba pesa. Siku moja alimwona Petro na Yohana wakiwa karibu kuingia hekaluni.

Picha
Mitume wakizungumza na mtu

Aliwaomba Petro na Yohana pesa. Petro alisema kwamba hakuwa na pesa yoyote. Petro alisema kwamba angempa mtu yule kitu kingine.

Picha
Petro akimsaidia mtu kusimama

Petro alimbariki mtu yule katika jina la Yesu Kristo na kumponya. Kisha alimsaidia yule mtu kusimama wima.

Picha
Petro akimsaidia mtu kutembea

Mtu yule alitembea kwa mara ya kwanza maishani mwake. Watu wengi walimuona mtu yule akitembea na kurukaruka. Walijua ulikuwa ni muujiza. Walijua Petro alikuwa na nguvu ya Mungu. Petro aliwaambia kwamba Yesu Kristo alikuwa amempa nguvu ya kumponya mtu yule. Petro alikuwa mmisionari mkuu. Aliwasaidia watu wengi kuamini katika Yesu Kristo na kumfuata.

Chapisha