Scripture Stories
Sura ya 2: Mariamu na Malaika


Sura ya 2

Mariamu na Malaika

Picha
Mariamu na Yusufu

Mariamu na Yusufu waliishi Nazareti. Walikuwa watu wema sana. Walipendana na walikuwa waoane.

Picha
malaika akizungumza na Mariamu

Siku moja malaika Gabrieli alimjia Mariamu. Alimwambia Mariamu kwamba Mungu angembariki.

Picha
malaika akizungumza na Mariamu

Gabrieli alimwambia Mariamu kwamba angekuwa mama wa Mwana wa Mungu. Jina lake lingekuwa Yesu, na angekuwa Mfalme wa watu wote wenye haki.

Picha
malaika akizungumza na Mariamu

Mariamu alisema kwamba angemtii Baba wa Mbinguni na kuwa mama wa Yesu.

Chapisha