Scripture Stories
Sura ya 21: Yesu Anaamuru Upepo na Mawimbi


Sura ya 21

Yesu Anaamuru Upepo na Mawimbi

Picha
mashua kwenye bahari yenye tufani

Yesu na wanafunzi Wake walikuwa katika mashua kwenye Bahari ya Galilaya. Yesu alilala. Upepo ulianza kuvuma kwa nguvu, na mawimbi yalikuwa yakijaza mashua kwa maji. Wanafunzi walikuwa na hofu kwamba ingezama. Walimwamsha Yesu na kumsihi asaidie.

Picha
Yesu akiamuru tufani

Mwokozi aliamuru upepo ukome kuvuma na mawimbi yatulie. Upepo ulikoma, na bahari ikatulia.

Picha
Yesu akiwafundisha wanafunzi

Yesu aliwauliza wanafunzi ni kwa nini walikuwa na hofu. Alisema kwamba walipaswa kuwa na imani zaidi. Walishangaa ni mtu wa aina gani anayeweza kuamuru hata upepo na bahari.

Chapisha