Scripture Stories
Sura ya 11: Yesu Ajaribiwa


Sura ya 11

Yesu Ajaribiwa

Picha
Yesu akiwa nyikani

Yesu alienda nyikani ili kuwa na Mungu. Mwokozi alizungumza na Baba wa Mbinguni. Hakula chochote kwa siku 40 kwa sababu Yeye alikuwa amefunga.

Mathayo 4:1–2 (ona rejeo chini ya ukurasa 1b na 2c); Luka 4:1–2 (ona rejeo chini ya ukurasa 2a)

Picha
Yesu akiwa nyikani

Ibilisi alikuja na kumjaribu Yesu kuthibitisha kwamba Yeye alikuwa Mwana wa Mungu. Kwanza, alimwambia Yesu abadili mawe yawe mkate. Yesu alikuwa na njaa, lakini alijua kwamba alipaswa tu kutumia nguvu Zake kuwasaidia watu wengine. Hakufanya kile ibilisi alichosema.

Mathayo 4:2–4; Yesu Kristo, 128–29

Picha
Yesu akiwa juu ya paa la hekalu

Kilichofuatia Roho Mtakatifu alimpeleka Yesu mahali pa juu hekaluni. Ibilisi alimjaribu Yesu mara ya pili, akimwambia aruke kutoka ukuta wa hekalu. Ibilisi alisema kwamba ikiwa Yesu alikuwa Mwana wa Mungu, malaika wasingemwacha Yeye aumie. Yesu hakuruka. Alijua kwamba ingekuwa makosa kutumia nguvu Zake takatifu kwa njia hii.

Mathayo 4:5–7 (ona rejeo chini ya ukurasa 5a na 6a)

Picha
Yesu akiwa nyikani

Kisha Roho Mtakatifu alimpeleka Yesu kwenye kilele cha mlima. Alimwonyesha Yesu falme zote na hazina zote za dunia. Ibilisi alimwambia Yesu kwamba angetwaa vitu hivi vyote kama angemtii. Yesu aliseme angemtii Baba wa Mbinguni pekee. Alimwambia ibilisi aondoke. Ibilisi aliondoka. Malaika walikuja na kumbariki Yesu. Yesu alikuwa tayari kuanza kazi Yake.

Mathayo 4:8–11 (ona rejeo chini ya ukurasa 8a na 9a)

Chapisha