Scripture Stories
Sura ya 15: Mwanamke Kisimani


Sura ya 15

Mwanamke Kisimani

Picha
Yesu akisafiri

Yesu aliondoka Yerusalemu kwenda Galilaya. Alisafiri kupitia Samaria na kufika kisimani.

Picha
Yesu akizungumza na mwanamke

Alikuwa amechoka, na alipumzika kisimani. Mwanamke Msamaria alikuja kuchota maji. Yesu alimwomba ampe maji anywe.

Picha
mwanamke amesimama

Kwa vile Wayahudi kwa kawaida hawakuzungumza na Wasamaria, mwanamke alishangazwa.

Picha
Yesu akizungumza

Yesu alimwambia mwanamke yule kwamba angempa aina ya maji ambayo yangemfanya asiwe na kiu kamwe. Alielezea kwamba Yeye alikuwa Mwokozi. Maji ambayo angempa yalikuwa “maji ya uzima” ya uzima wa milele.

Picha
mwanamke akizungumza na watu

Mwanamke alienda mjini na kuwaambia watu wengi kuhusu Yesu. Walienda kisimani na kumsikiliza Yesu wao wenyewe. Wengi wao waliamini maneno Yake.

Chapisha