Sura ya 54 Yesu Amefufuka Mwili wa Mwokozi ulikuwa kaburini hadi Jumapili asubuhi. Kisha malaika wawili walikuja na kulivingirisha jiwe kutoka kwenye kaburi. Mathayo 28:1–2 (ona rejeo chini ya ukurasa 2a); Luka 24:1–4 Mwanamke ambaye Yesu alikuwa amemponya aliyeitwa Mariamu Magdalene alienda kaburini. Alistaajabu kuona kwamba jiwe lilikuwa limeondolewa. Mwili wa Yesu haukuwa kaburini. Yohana 20:1–2 Alikimbia kuwaambia Petro na Yohana kwamba mtu alikuwa ameuchukua mwili wa Mwokozi. Hakujua pale ulipokuwa. Yohana 20:2 Petro na Yohana walikimbia kwenda kaburini. Walikuta kitambaa ambacho Yesu alikuwa amezikwanacho, lakini mwili wa Yesu haukuwepo. Petro na Yohana hawakujua nini cha kufanya. Walienda nyumbani. Yohana 20:3–7, 10 Mariamu Magdalene alibaki kaburini, akilia. Alipotazama ndani ya kaburi tena, aliwaona malaika wawili. Yohana 20:11–12 Walimwuuliza Mariamu Magdalene kwa nini alikuwa akilia. Alisema mtu alikuwa ameuchukua mwili wa Yesu. Hakujua pale ulipokuwa. Yohana 20:13 Aligeuka na kumwona mtu. Alidhani alikuwa mtunza bustani. Alimuliza kwa nini alikuwa akilia. Alimuuliza Yeye kama alikuwa anajua pale mwili wa Yesu ulipokuwa. Yohana 20:14–15 Kisha mtu yule akasema, “Mariamu,” na alijua alikuwa ni Yesu. Alimsihi awaeleze Mitume kwamba Yeye alikuwa amefufuka. Yohana 20:15–17 Mariamu Magdalene na wanawake wengine waliwaambia Mitume kwamba Yesu alikuwa amefufuka. Mara ya kwanza Mitume hawakuwaamini. Luka 24:10–11; Yohana 20:18 Baadaye, wakati Mitume walipokuwa wakizungumza kati yao, Yesu alikuja chumbani. Mitume waliogopa. Bado walidhani Yeye amekufa. Luka 24:36–37 Mwokozi aliwaambia waguse mikono na miguu Yake. Alikuwa amefufuka—mwili na roho Yake vilikuwa vimeungana tena. Luka 24:38–40 Mitume walikuwa na furaha kumwona Yeye. Aliwaomba wampe chakula. Walimpa samaki na sega la asali. Alikula. Luka 24:41–43 Yesu Kristo alikuwa ndiye mtu wa kwanza kufufuka. Wengi wengine walifufuliwa na kuonekana na watu walioishi Yerusalemu. Yesu alikuwa amesema, “Mimi ndiye ufufuo, na uzima.” Kwa sababu alishinda kifo, sote tutafufuliwa siku moja. Mathayo 27:52–53; Yohana 11:25