Sura ya 39 Yesu Anamponya Kipofu Siku moja Yesu alikuwa akitembea na wanafunzi Wake. Walimwona mtu aliyekuwa amezaliwa kipofu. Wanafunzi waliuliza kama mtu yule alikuwa kipofu kwa sababu alikuwa ametenda dhambi ama kwa sababu wazazi wake walikuwa wametenda dhambi. Yohana 9:1–2 Mwokozi alisema kwamba si wazazi wala mtu yule aliyekuwa ametenda dhambi. Mtu yule alikuwa kipofu ili kwamba Yesu amponye na kuonyesha watu nguvu ya Mungu. Yohana 9:3–5 Yesu alitengeneza matope kutoka kwenye udongo. Akayaweka kwenye macho ya kipofu. Yesu alimwambia mtu yule aende akaoshe macho yake. Yohana 9:6–7 Mara tu mtu yule alipoosha matope kutoka kwenye macho yake, aliona! Yohana 9:7 Jirani zake walipomuona, hawakuwa na uhakika yeye ni nani. Aliwaambia kwamba Yesu alikuwa amemponya. Majirani walimpeleka mtu yule kwa Mafarisayo. Mtu yule aliwaambia Mafarisayo kwamba Yesu alikuwa amemponya. Yohana 9:8–11 Baadhi ya Mafarisayo walifikiri Yesu lazima awe mtu mwadilifu. Wengine walifikiri Yeye alikuwa mwenye dhambi. Mtu yule aliposema Yesu alikuwa mtu mwadilifu, baadhi ya Mafarisayo walikasirika na kumtoa mtu huyo nje. Yohana 9:13–16, 30–34 Yesu alimpata mtu yule. Alimuuliza kama aliamini katika Mwana wa Mungu. Mtu yule aliuliza Mwana wa Mungu ni nani. Yesu alisema kwamba Yeye alikuwa Mwana wa Mungu, na mtu yule akamwabudu. Yohana 9:35–38