Scripture Stories
Sura ya 28: Yesu Anawalisha Watu 5,000


Sura ya 28

Yesu Anawalisha Watu 5,000

Picha
watu wakizungumza na Yesu

Baadhi ya rafiki za Yohana Mbatizaji walimwambia Yesu kwamba Yohana alikuwa ameuwawa na mfalme.

Picha
Yesu amekaa juu ya jiwe

Yesu aliposikia haya, alienda mahali karibu na Bahari ya Galilaya ili awe peke yake. Watu wengi walijua kule alikokuwa. Zaidi ya watu 5,000 walimfuata kule wakitumaini kwamba Yeye angewafundisha.

Picha
mtu akizungumza na Yesu

Yesu aliwafundisha mambo mengi. Ilikuwa muda wa kula, lakini wengi wa watu wale hawakuwa na chakula chochote. Wanafunzi wake walimtaka Yesu awatume watu kwenye kijiji kilichokuwa karibu kununua chakula.

Picha
mvulana akileta chakula kwa Yesu

Yesu aliwaambia wanafunzi watafute ikiwa kuna yeyote aliyekuja na chakula. Walimpata mvulana aliyekuwa na mikate mitano na samaki wawili wadogo.

Picha
Yesu akibariki chakula

Yesu aliwaambia watu wote waketi chini. Alibariki mikate na samaki na kumega chakula kwenye vipande.

Picha
wanafunzi wakigawa chakula

Wanafunzi waliwapa watu chakula. Kulikuwa na zaidi ya kutosha kwa kila mmoja.

Chapisha