Scripture Stories
Sura ya 9: Mvulana Yesu


Sura ya 9

Mvulana Yesu

Picha
Kijana Yesu akisali

Yesu alilelewa katika mji wa Nazareti. Alijifunza mambo mengi na “akaongezeka nguvu, … na neema ya Mungu ilikuwa juu yake.”

Picha
Kijana Yesu akisafiri na watu

Yesu alipokuwa na miaka 12, Alienda na Yusufu na Mariamu katika kikundi cha watu kwenye sherehe Yerusalemu. Walikuwa huko kwa siku kadhaa.

Picha
Yusufu na Mariamu wakisafiri

Wakati Yusufu na Mariamu walipoondoka kwenda nyumbani, walifikiria kwamba Yesu alikuwa akitembea kurudi Nazareti pamoja na rafiki Zake. Lakini Yesu alikuwa amebaki Yerusalemu.

Picha
Yusufu na Mariamu wakizungumza na watu

Wakati Yusufu na Mariamu walipomtafuta Yesu, hawakuweza kumpata. Hakuna yeyote katika kikundi chao aliyekuwa Amemwona. Hivyo Yusufu na Mariamu walirudi Yerusalemu. Walimtafuta Yesu kwa siku tatu. Walihuzunika sana.

Picha
Kijana Yesu akiwafundisha watu

Hatimaye walimpata Yesu Hekaluni, akizungumza na baadhi ya walimu. Alikuwa akijibu maswali yao. Walimu walishangazwa na mengi ambayo Yesu aliyajua.

Luka 2:46–47 (ona rejeo chini ya ukurasa 46c)

Picha
Kijana Yesu akizungumza na Mariamu na Yusufu

Mariamu alimwambia Yesu kwamba yeye na Yusufu walikuwa na hofu kumhusu Yeye. Yesu alijibu kwamba alikuwa akifanya kazi ya Baba Yake — kazi ya Mungu. Yusufu na Mariamu hawakuelewa.

Picha
Yusufu, Mariamu, na kijana Yesu wakisafiri

Yesu alienda nyumbani Nazareti pamoja na Yusufu na Mariamu na kuwatii.

Picha
Kijana Yesu akisoma

Yesu alijifunza zaidi na zaidi kuhusu kazi ya Baba Yake wa Mbinguni.

Picha
Kijana Yesu akitengeneza upinde

Alikuwa mrefu na mwenye nguvu.

Picha
Kijana Yesu akiwasaidia watu

Watu walimpenda. Alifanya kile Mungu alimtaka Yeye afanye.

Picha
Kijana Yesu akisali

Mungu Alimpenda.

Chapisha