Picha za Nchi Takatifu (Namba katika mabano ni namba za sura za hadithi ambazo zilitendeka mahali ama karibu na mahali picha ilipochukuliwa. ) BethlehemuYesu Kristo alizaliwa katika mji huu. (5, 7) HekaluHuu ni mfano wa hekalu katikaYerusalemu ambapo Yesu alifundisha injili na kuwafukuza nje watu waliokuwa wakiuza wanyama kwa ajili ya dhabihu. (1, 6, 9, 11, 13, 45, 56) Ngazi za kwenda HekaluniHizi ni ngazi halisi zilizoelekeza hekaluni. NazaretiYesu alilelewa katika mji huu. (2, 4, 9, 17) YerusalemuYesu na Mitume Wake walitumia muda mwingi kufundisha katika mji huu. Yesu alikufa na kufufuka hapa. (6, 39–40, 44–57, 63) Mto YordaniYohana Mbatizaji alimbatiza Yesu Kristo mahali fulani katika mto huu. (10) Nyika za YudeaYesu Kristo alifunga na kujaribiwa na ibilisi nyikani baada ya ubatizo Wake. (11) SamariaYesu alimfundisha mwanamke kuhusu maji ya uzima kisimani katika nchi hii. Wengi wa Wayahudi waliwachukia watu wa Samaria. (15, 58) Galilaya na Bahari ya GalilayaWatu wengi wanaamini upande huu wa mlima ndipo mahali Yesu alitoa Mahubiri ya Mlimani. Bahari ya Galilaya iko kwa nyuma. Yesu alifundisha injili kwa watu wengi, ikijumuisha Mitume Wake, karibu na hapa. Yesu alituliza dhoruba kwenye Bahari ya Galilaya. (18–22, 29, 34, 36) KapernaumuMagofu haya yako katika mji wa Kapernaumu. Yesu alifanya miujiza mingi katika mji huu. (23–25, 30) Kaisaria FilipiKatika eneo hili Yesu alishuhudia kifo Chake na Ufufuko Wake, na Petro alishuhudia kwamba Yesu ndiye Mwana wa Mungu. (32) YerikoKatika fumbo la Msamaria mwema, mtu alikaribia kuuwawa alipokuwa akisafiri njiani kwenda kwenye mji huu. (35) Mlima TaboriHapa huenda ni mahali ambapo kugeuzwa kwa Yesu Kristo kulitokea. (33) Bustani ya GethsemaneYesu Kristo aliomba, aliteseka kwa ajili ya dhambi zetu, alisalitiwa na Yuda Iskariote, na alikamatwa katika bustani hii. (51, 52) GolgothaHapa huenda pakawa mahali ambapo Yesu Kristo alikufa msalabani. (53) Kaburi la BustaniHapa huenda ni mahali ambapo Yesu Kristo alizikwa, alifufuka, na kuzungumza na Mariamu Magdalene. (53, 54)