Scripture Stories
Sura ya 33: Kuonekana katika Utukufu: Kugeuzwa


Sura ya 33

Kuonekana katika Utukufu: Kugeuzwa

Picha
Yesu, Petro, Yakobo, na Yohana wakitembea

Yesu aliwachukua Petro, Yakobo, na Yohana kwenye kilele cha mlima kusali.

Picha
Musa na Eliya wakimtokea Yesu

Yesu alipokuwa akisali, utukufu wa Mungu ulikuja juu Yake. Uso wake uling’aa kama jua. Manabii wawili wa Agano la Kale walioitwa Musa na Eliya walimjia. Walizungumza kuhusu kifo na ufufuo Wake uliokuwa unakuja.

Mathayo 17:2–3; Marko 9:3–4; Luka 9:29–31 (ona rejeo chini ya ukurasa 31a)

Picha
Petro, Yakobo, na Yohana wamelala

Yesu alipokuwa akisali, Mitume walilala.

Picha
Yesu, Musa, na Eliya wakiwatokea Mitume

Walipoamka, waliona utukufu wa Yesu Kristo, Musa, na Eliya. Walisikia sauti ya Baba wa Mbinguni ikishuhudia, “Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa Naye, msikieni yeye.”

Picha
Yesu akiwakaribia Mitume

Mitume walikuwa na hofu na wakaanguka chini. Yesu aliwagusa na kuwaambia wasiwe na hofu. Walipotazama juu, wajumbe wa mbinguni walikuwa wameondoka. Yesu aliwaambia Mitume wasimwambie yeyote kile walichokuwa wamekiona hadi baada ya kufa Kwake na kufufuka.

Chapisha