Scripture Stories
Sura ya 58: Simoni na Ukuhani


Sura ya 58

Simoni na Ukuhani

Picha
watu wakifundishwa

Watu wengi katika Samaria walisikia na kuamini injili. Walibatizwa, lakini hawakuwa na Roho Mtakatifu.

Picha
Mitume wakiweka mikono juu ya kichwa cha mtu

Petro na Yohana walikwenda Samaria. Waliweka mikono yao juu ya vichwa vya watu na kuwapa kipawa cha Roho Mtakatifu.

Picha
mtu akiwatazama Mitume

Mtu aliyeitwa Simoni aliwaona Petro na Yohana wakiwapa watu kipawa cha Roho Mtakatifu. Simoni alijua kwamba Mitume hao wawili waliweza kuwapa watu kipawa cha Roho Mtakatifu kwa sababu walikuwa na ukuhani. Alitaka ukuhani pia.

Picha
mtu akiwapa mitume pesa

Aliwatolea Petro na Yohana pesa wampe ukuhani. Petro alimwambia Simoni kwamba hakuna anayeweza kununua ukuhani. Mungu huwapa wanaume walio waadilifu. Petro alijua kwamba Simoni hakuwa mwadilifu. Alimwambia atubu.

Chapisha