Sura ya 47 Wanawali Kumi Yesu alisimulia hadithi kuhusu wasichana kumi walioenda kwenye harusi. Walimngoja bwana harusi aje na kuwakaribisha ndani. Hawakujua ni saa ngapi angekuja. Mathayo 25:1, 13 Wanawake hao kumi walikuwa na taa za mafuta. Watano kati yao walikuwa na busara. Walikuwa wamebeba mafuta ya ziada. Mathayo 25:2, 4 Wanawake wengine watano walikuwa wapumbavu. Walikuwa tu na mafuta yaliyokuwa ndani ya taa zao. Mathayo 25:3 Bwana harusi hakuja kwa muda mrefu. Mafuta ndani ya taa yaliisha. Wanawake watano wenye busara walikuwa na mafuta ya ziada ya kuweka ndani ya taa zao. Wanawake watano wapumbavu walilazimika kwenda kununua mafuta ya ziada. Mathayo 25:5–9 Walipokuwa wameenda, bwana harusi alikuja. Aliwakaribisha wanawake watano wenye busara kwenye harusi. Mathayo 25:10 Wakati wanawake watano wapumbavu waliporejea, mlango ulikuwa umefungwa. Hawangeweza kuingia kwenye harusi. Mathayo 25:10–12 Yesu ni kama bwana harusi katika hadithi hii. Waumini wa Kanisa ni kama wale wanawake kumi. Yesu atakapokuja tena, baadhi ya waumini watakuwa tayari. Watakuwa wametii amri za Mungu. Wengine hawatakuwa tayari. Hawataweza kuwa na Mwokozi atakapokuja tena. Mathayo 25:13; Mafundisho na Maagano 45:56–57; 88:86, 92; Yesu Kristo, 576–80