Scripture Stories
Sura ya 50: Mafundisho Mengine katika Mlo wa Mwisho


Sura ya 50

Mafundisho Mengine katika Mlo wa Mwisho

Picha
Yesu akizungumza

Walipomaliza kula, Yesu aliwaambia Mitume Wake kwamba walipaswa kupendana kama vile Yeye alivyowapenda. Kama wangefanya hivi, watu wangejua walikuwa wanafunzi Wake.

Picha
Yesu Akiwafundisha Mitume

Alisema kwamba ikiwa Mitume walimpenda, wangetii amri Zake. Aliwaahidi kipawa cha Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu angewafundisha kila kitu walichohitaji kujua. Roho Mtakatifu angewasaidia Mitume kukumbuka vitu ambavyo Yesu alikuwa amewafunza.

Picha
Yesu akizungumza

Yesu alisema kwamba Yeye alikuwa kama mzabibu. Wanafunzi Wake ni kama matawi ya mzabibu. Ni tawi ambalo tu limeunganishwa imara kwenye mzabibu linaweza kuzaa matunda mazuri.

Picha
Yesu akifundisha

Yesu aliwaahidi Mitume Wake kwamba kama wakiishi injili, matunda yao (matendo yao) yangekuwa mema. Kama hawangemfuata Yeye, wangekuwa kama matawi yaliyokatwa kutoka kwenye mmea na kutozaa chochote.

Picha
Yesu akisali

Yesu Kristo aliomba kwamba Mitume Wake wangekuwa na umoja. Aliwataka wawafundishe watu kumwamini Yeye na kujua kwamba Baba wa Mbinguni anawapenda.

Picha
Yesu na Mitume wakiimba

Kisha Yesu na Mitume waliimba wimbo na kuondoka chumbani.

Chapisha