Scripture Stories
Sura ya 25: Mwanamke Anagusa Mavazi ya Yesu


Sura ya 25

Mwanamke Anagusa Mavazi ya Yesu

Picha
mwanamke mgonjwa amelala kitandani

Mwanamke alikuwa mgonjwa sana kwa miaka 12. Alikuwa ameenda kwa madaktari wengi, lakini hawakuweza kumsaidia.

Picha
mwanamke akigusa vazi la Yesu

Siku moja alimwona Yesu akiwa amezingirwa na watu wengi. Aliamini kwamba angeponywa kwa kugusa tu vazi Lake. Alitembea katikati ya umati na kugusa vazi Lake.

Picha
mwanamke akitoa tabasamu kwa Yesu

Aliponywa mara moja. Yesu aligeuka na kuuliza, “Ni nani aliyegusa mavazi yangu?”

Picha
mwanamke amepiga magoti

Mwanamke alikuwa na hofu. Alipiga magoti mbele ya Mwokozi na kusema kwamba alikuwa amemgusa. Yesu alimwambia kwamba imani yake Kwake ilimponya.

Chapisha