Scripture Stories
Sura ya 22: Mtu Mwenye Mapepo wachafu


Sura ya 22

Mtu Mwenye Mapepo wachafu

Picha
mtu akiwa katika minyororo iliyokatika

Mtu aliyeishi makaburini kando ya Bahari ya Galilaya alikuwa na pepo wachafu ndani yake ambao walimfanya awe na tabia ya wenda wazimu. Watu walimfunga na minyororo ili kumdhibiti, lakini aliikata minyororo.

Picha
mtu ameshikilia jiwe

Mtu yule alishinda siku nzima na usiku mzima kwenye milima na mapango. Alilia siku zote na kujikata kata kwa mawe.

Picha
Yesu akimsogelea mtu

Siku moja Yesu na wanafunzi Wake walivuka Bahari ya Galilaya kwenye mashua. Mwokozi aliposhuka kutoka kwenye mashua, mtu yule alimkimbilia.

Picha
Yesu akizungumza na mtu

Yesu aliliambia pepo limtoke mtu huyo. Pepo lilijua Yesu alikuwa Mwana wa Mungu. Lilimsihi Yesu asilitese.

Picha
mtu mwoga

Mwokozi alipoliuliza pepo jina lake lilikuwa nani, lilisema, “Jina langu ni Legioni,” ikimaanisha wengi. Mapepo mengi wachafu walikuwa ndani ya mtu yule. Walimsihi Yesu awaruhusu waingie ndani ya miili ya baadhi ya nguruwe waliokuwa karibu.

Picha
Nguruwe wakikimbilia baharini

Yesu alikubali. Mapepo yalimtoka mtu yule na kwenda katika miili ya takribani nguruwe 2,000. Nguruwe walikimbia chini ya mlima hadi ndani ya bahari na kuzama.

Picha
mtu akizungumza na watu

Watu waliokuwa wakichunga nguruwe walikimbia mjini na kuwaambia watu kile kilichokuwa kimetokea. Watu walikuja na kumuona Yesu na yule mtu aliyekuwa mwenda wazimu. Lakini mtu yule hakuwa mwenda wazimu tena.

Picha
watu wakizungumza na Yesu

Hii iliwafanya watu wamwogope Yesu. Walimsihi Yeye aondoke. Alirudi kwenye mashua.

Picha
mtu akimwangalia Yesu akiondoka na mashua

Mtu aliyeponywa alitaka aondoke pamoja Naye. Badala yake Mwokozi alimwambia aende nyumbani na awaambie rafiki zake kile kilichomtokea.

Picha
mtu akizungumza na watu

Mtu yule aliwaambia rafiki zake, na walishangazwa na uwezo mkubwa wa Yesu.

Chapisha