Scripture Stories
Sehemu za Kujua


Sehemu za Kujua

(Namba katika mabano ni sura ambazo zinaeleza kuhusu matukio ambayo yaliyotokea katika sehemu hizi.)

Ramani ya 1: Nchi Takatifu katika Nyakati za Agano Jipya

  1. DameskiPaulo alikuwa akienda kwenye mji huu wakati Yesu alipomtokea na kumwambia atubu. (59)

  2. Kaisaria FilipiKatika eneo hili Yesu alishuhudia kifo Chake na Ufufuko Wake, na Petro alishuhudia kwamba Yesu ndiye Mwana wa Mungu. (32)

  3. GalilayaYesu alitumia muda mwingi katika eneo hili akifundisha injili na kuponya wagonjwa. (19–20, 34, 36)

  4. KapernaumuYesu alifanya miujiza mingi katika mji huu. (23–25, 30)

  5. Bahari ya GalilayaYesu alifundisha injili kwa watu wengi karibu na hapa. Yesu alituliza dhoruba na kutembea juu ya maji ya Bahari ya Galilaya. (18, 21, 29)

  6. KanaYesu alibadili maji kuwa divai kwenye karamu ya harusi hapa. Mtu alikuja hapa kumwomba Yesu amponye mwanawe mgonjwa. (12, 16)

  7. NazaretiYesu alilelewa katika mji huu. (2, 4, 9, 17)

  8. SamariaYesu alimfundisha mwanamke kuhusu maji ya uzima kisimani katika nchi hii. Wengi wa Wayahudi waliwachukia watu wa Samaria. (15, 58)

  9. Mto YordaniYohana Mbatizaji alimbatiza Yesu Kristo kwenye mto huu.

  10. YafaPetro alimfufua Tabitha hapa. (60)

  11. YerikoKatika fumbo la Msamaria mwema, mtu alikaribia kuuwawa alipokuwa akisafiri njiani kwenda kwenye mji huu. (35)

  12. YerusalemuYesu na Mitume Wake walitumia muda mwingi kufundisha katika mji huu. Yesu alikufa na kufufuka hapa. (6, 39–40, 44–57, 63) Ona Ramani ya 2 kwa hadithi za ziada ambazo zilitokea Yerusalemu.

  13. BethaniaLazaro, ambaye Yesu alimfufua, aliishi hapa na dada zake Mariamu na Martha. (43)

  14. BethlehemuYesu Kristo alizaliwa hapa. (5, 7)

Bahari ya Kati

Bahari ya Chumvi

Dameski

Kaisaria Filipi

GALILAYA

Kapernaumu

Bahari ya Galilaya

Kana

Nazareti

SAMARIA

Mto Yordani

Yafa

Yeriko

Yerusalemu

Bethania

Bethlehemu

Ramani ya 2: Yerusalemu katika wakati wa Yesu

  1. GolgothaHapa huenda pakawa mahali ambapo Yesu Kristo alikufa msalabani. (53)

  2. Kaburi la BustaniHapa huenda ni mahali ambapo Yesu Kristo alizikwa, alifufuka, na kuzungumza na Mariamu Magdalene. (53, 54)

  3. Bwawa la BethzathaYesu alimponya mtu siku ya Sabato hapa. (27)

  4. HekaluHapa malaika Gabrieli alimuahidi Zakaria kwamba angepata mwana, ambaye alikuwa Yohana Mbatizaji. Yesu alifundisha katika hekalu hili. Pia aliwafukuza watu nje ya hekalu ambao walikuwa wakiuza wanyama wa kutoa dhabihu. (1, 6, 9, 11, 13, 45, 56)

  5. Bustani ya Gethsemane Yesu Kristo alisali, aliteseka kwa ajili ya dhambi zetu, alisalitiwa na Yuda Iskariote, na alikamatwa katika bustani hii. (51, 52)

  6. Mlima wa MizeituniYesu alifundisha kuhusu Ujio Wake wa Pili hapa. (46)

  7. Nyumba ya KayafaHapa huenda pakawa mahali ambapo viongozi wa Kiyahudi walimshitaki Yesu, wakimshutumu kwa kuvunja sheria. (52)

  8. Chumba cha JuuChumba ambapo Yesu na Mitume Wake walikula Pasaka huenda ilikuwa katika eneo hili. Yesu aliwafundisha Mitume Wake kuhusu sakramenti muda mfupi kabla ya kwenda kwenye Bustani ya Gethsemane. (49, 50)

Golgotha

Kaburi la Bustani

Bwawa la Bethzatha

Hekalu

Bustani ya Gethsemane

Mlima wa Mizeituni

Nyumba ya Kayafa

Chumba cha Juu

Chapisha