Sura ya 12 Harusi huko Kana Yesu Kristo na wanafunzi Wake walihudhuria karamu ya harusi huko Kana. Mariamu, mama wa Yesu, alikuwa huko. Alimwambia Yesu kwamba hakukuwa na divai kwa ajili ya wageni. Yohana 2:1–3 Yesu alimheshimu na kumpenda mama Yake. Alimuuliza kile alichotaka Yeye afanye. Yohana 2:4 (ona rejeo chini ya ukurasa 4a) Mariamu aliwaambia watumishi kwenye harusi wafanya chochote ambacho Yesu aliwaambia wafanye. Yohana 2:5 Yesu aliwaambia watumishi wajaze mitungi sita mikubwa ya mawe kwa maji. Kila mtungi ulijaa kati ya galoni 18 na 27 (lita 68 na 102). Kisha alibadilisha maji kuwa divai. Yohana 2:6–7 Aliwaambia watumishi watoe divai kutoka kwenye mitungi na wampatie mtawala wa karamu. Yohana 2:8 Mtawala wa karamu alishangazwa alipokunywa divai. Divai bora kwa kawaida ilitolewa mwanzoni mwa karamu. Lakini wakati huu, divai bora ilitolewa mwisho. Yohana 2:9–10 Huu ni muujiza wa kwanza kuwekwa kumbukumbu ambao Yesu alifanya wakati wa maisha yake duniani. Aliufanya ili kumsaidia mama Yake. Ulisaidia pia kuimarisha imani ya wanafunzi Wake. Yohana 2:11