Sura ya 43 Yesu Anamfufua Lazaro Mtu aliyeitwa Lazaro aliishi Bethania na dada zake Mariamu na Martha. Yesu alimpenda Lazaro na dada zake, na wao walimpenda Yesu. Yohana 11:1–2, 5 Lazaro akawa mgonjwa sana. Mwokozi alikuwa katika mji mwingine. Mariamu na Martha walituma ujumbe Kwake kwamba Lazaro alikuwa mgonjwa. Yohana 11:3 Mwokozi aliwaambia wanafunzi Wake waende Naye kumsaidia Lazaro. Wanafunzi walikuwa na hofu kwenda Bethania. Ilikuwa karibu na Yerusalemu. Baadhi ya watu huko Yerusalemu walitaka kumwua Yesu. Yohana 11:6–8, 18 Yesu aliwaambia wanafunzi Wake kwamba Lazaro alikuwa amekufa. Alisema kwamba Yeye angemfufua. Muujiza huu ungewasaidia wanafunzi kujua kwamba Yeye alikuwa Mwokozi. Yesu alienda Bethania. Alipofika huko, Lazaro alikuwa amekufa kwa siku nne. Yohana 11:11–17, 19 Martha alimwambia Yesu kwamba Lazaro angelikuwa bado hai kama Yeye angelikuja mapema. Yesu alisema Lazaro angeishi tena. Alimuuliza Martha kama alimuamini. Martha alisema ndio. Alijua kwamba Yesu alikuwa Mwokozi. Yohana 11:20–27 Martha alimuacha Yesu na kwenda kumwita dada yake, Mariamu. Mariamu alienda kukutana na Yesu pia. Watu wengi walimfuata. Mariamu alipiga magoti, akilia, miguuni pa Mwokozi. Watu waliokuwa naye walikuwa wakilia pia. Yesu aliuliza mahali mwili wa Lazaro ulipokuwa. Yohana 11:28–34 Yesu alienda kwenye pango ambamo Lazaro alikuwa amezikwa. Kulikuwa na jiwe mbele yake. Aliwaambia watu wasogeze jiwe. Yohana 11:38–39 Yesu alitazama juu. Alimshukuru Baba wa Mbinguni kwa kusikiliza maombi Yake. Yohana 11:41–42 Kisha, kwa sauti kubwa, Yesu alimwambia Lazaro atoke pangoni. Lazaro alitoka nje. Watu wengi walioona muujiza huo sasa waliamini kwamba Yesu alikuwa Mwokozi. Yohana 11:43–45