Scripture Stories
Sura ya 63: Paulo Anahitimisha Utume Wake


Sura ya 63

Paulo Anahitimisha Utume Wake

Picha
watu wakimpigia kelele Paulo

Paulo alienda hekaluni huko Yerusalemu. Kundi la Wayahudi lilifikiri Paulo alikuwa amewaleta watu ambao hawakuwa Wayahudi hekaluni. Hili liliwakasirisha Wayahudi. Walimtoa Paulo nje ya hekalu na kumpiga.

Picha
askari wamesimama kando ya Paulo

Askari wa Rumi walimkamata Paulo. Walimwacha azungumze na Wayahudi. Paulo alishuhudia kwa watu kwamba alikuwa ameona nuru kutoka mbinguni na kusikia sauti ya Mwokozi. Alisema kwamba Yesu alikuwa amemwambia ahubiri injili.

Picha
askari wakimuondosha Paulo

Watu hawakumwamini Paulo. Walitaka kumwua. Askari walimweka Paulo gerezani kwa usiku ule.

Picha
Mwokozi akimtokea Paulo

Mwokozi alimtembelea Paulo gerezani na kumwambia asiogope. Alisema Paulo angeenda Roma na kufundisha injili huko.

Picha
Paulo akiwafundisha watu

Ili kumlinda Paulo, Warumi walimpeleka kwenye mji mwingine. Mfalme Agripa alikuwa huko. Paulo alimwambia Mfalme Agripa kwamba alikuwa Mfarisayo na alikuwa akiwachukia watu walioamini katika Yesu. Alikuwa hata akiwaweka gerezani. Kisha Paulo alikuwa ameona nuru kutoka mbinguni na kusikia sauti ya Mwokozi. Sasa aliamini katika Yesu.

Picha
Paulo akimfundisha Mfalme Agripa

Paulo alishuhudia kwa Mfalme Agripa kwamba injili ilikuwa kweli. Alisema kwamba Yesu alikuwa amefufuka. Katika ono, Yesu Kristo alikuwa amemwambia Paulo afundishe injili Yake. Kwa sababu Paulo alikuwa ametii, watu wengi walimchukia Paulo.

Picha
askari wakimuongoza Paulo kwenye mashua

Mfalme Agripa alisema kwamba Paulo karibu amfanye aamini katika Yesu. Mfalme hakufikiri Paulo alipaswa kuuwawa. Lakini ilimbidi ampeleke Paulo hadi Roma, ambapo Paulo angeshitakiwa.

Picha
Paulo akiandika kwenye hati ya kukunja

Paulo alikuwa gerezani huko Roma kwa miaka miwili. Watu wengi walikuja kumuona. Aliwafundisha injili. Paulo aliandika barua kwa Watakatifu katika nchi zingine. Baadhi ya barua hizi, zilizoitwa nyaraka, ziko katika Agano Jipya.

Picha
Paulo akiomba

Paulo alijua angeuwawa. Hakuogopa. Alikuwa ametii amri za Mungu. Alikuwa amefundisha injili. Alikuwa amehitimisha utume wake. Paulo alijua kwamba Baba wa Mbinguni alimpenda. Alijua pia kwamba baada ya kufa, angeishi na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo.

Chapisha